Netflix kuwekeza zaidi ya Tsh Trilioni 17 katika filamu na tamthilia mpya 2018

0
Sambaza

Kampuni ya huduma ya TV ya kimtandao, Netflix, ipo njiani kuendelea kuwekeza zaidi katika filamu na tamthilia zake kwa mwaka 2018.

Wametangaza rasmi kukusanya mtaji mwingine wa dola bilioni 1.6 za Marekani (zaidi ya trilioni 2.5 za Kitanzania) na hivyo idadi nzima kuwa dola bilioni 8 kama bajeti nzima kwa ajili ya utengenezaji wa vipindi kwa mtandao wao. Hii ni mjumuisho wa filamu, tamthilia na vipindi vingine mbalimbali.

netflix kuwekeza Tsh trilioni 17

Netflix ni nini?

Netflix ni huduma namba moja duniani ya kukupatia video za filamu na tamthilia kwa njia ya kuzitazama kupitia huduma ya intaneti, kimombo ‘streaming’.

Je ni bure?

Hapana, kuna vifurushi kadhaa ila kifurushi cha kuanzia ni dola $7.99 (Takribani Tsh 17,504/= au Kes 816/=). – Kuifahamu zaidi huduma ya Netflix – Netflix ni nini?

Kwa mwaka 2018 mtaji mzima wa utengenezaji vipindi utakuwa dola bilioni 8 za Marekani – zaidi ya trilioni 17.9 za Kitanzania.

Narcos, Moja ya show maarufu iliyotengenezwa na Netflix

Mtandao wa Netflix umezidi kuongeza watumiaji, hadi sasa una watumiaji zaidi ya milioni 109 (Watumiaji zaidi ya milioni 15.5 ni wapya kwa mwaka huu).

SOMA PIA:  Firefox Send: Mozilla waja na huduma ya kutuma mafaili kwa usiri

Huduma za kimtandao zinazidi kupamba moto na kupata mafanikio makubwa duniani kote, na sasa tunazidi kuona biashara hizi za kimtandao mpya zikizidi kukua na kuwa na nguvu kubwa kipesa hata kuzidi huduma zingine zilizokuwepo kwa miaka mingi.

Vipi je ushawahi kujaribu huduma ya Netflix?

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com