Netflix yafikisha watumiaji milioni 100

1
Sambaza

Huduma ya kuangalia filamu na tamthilia mitandaoni ya Netflix yafikisha watumiaji milioni 100.

Mtandao wa Netflix ambao unashindana moja kwa moja dhidi ya makampuni mengine yanayotoa huduma za Tv kama vile DSTV na Azama TV kwenye soko letu imejikuta ikiendelea kupata mafanikio makubwa katika kuvutia watumiaji wapya.
Katika data mpya walizotoa imeoonesha wamefikisha watumiaji milioni 104 na huku zaidi ya nusu yao wakiwa wakitokea katika mataifa mengine nje ya Marekani – hii ni mara ya kwanza kwa watumiaji kutoka mataifa nje ya Marekani kuwa wengi zaidi.
 Netflix yafikisha watumiaji milioni 100

Narcos, Moja ya show maarufu iliyotengenezwa na Netflix

Netflix ni nini?

Netflix ni huduma namba moja duniani ya kukupatia video za filamu na tamthilia kwa njia ya kuzitazama kupitia huduma ya intaneti, kimombo ‘streaming’.

SOMA PIA:  YouTube GO - App ya YouTube isiyokula data sana

Badala ya kushusha (download) utaweza tazama filamu mbalimbali mpya na za zamani moja kwa moja kwenye simu, tableti au kompyuta yako.

Je ni bure?

Hapana, kuna vifurushi kadhaa ila kifurushi cha kuanzia ni dola $7.99 (Takribani Tsh 17,504/= au Kes 816/=). Kufahamu zaidi somo makala yetu hapa -> Netflix ni nini?

Wengi wanaamini kwa jinsi Netflix wanavyozidi kuwekeza katika kuleta filamu na tamthilia mpya za kisasa zaidi na huku wenyewe pia wakiwekeza katika filamu zao basi ndio ukuaji wao utazidi kuongezeka.

Je ushawahi kutumia huduma ya Netflix? Tupe maoni yako juu ya huduma hii.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com