Nguruwe kutumika kutibu upofu! #Sayansi #China

0
Sambaza

Wanasayansi wa Uchina wamefaulu katika tiba yao mpya ya majaribio ya kutibu upofu.

Walitumia Nguruwe katika majaribio hayo ya tiba ya kuondoa upofu, ambapo walitumia kornea kutoka kwa wanyama hao na kuweka kwenye macho ya binadamu.

Nguruwe

Kornea kutokwa kwa nguruwe hutibiwa na kutolewa DNA kabla ya kupandikizwa

Sasa wamesema wana imani kwamba hilo litafaa sana kutokana na uhaba wa kornea za binadamu. Inakisiwa kuwa Wachina wapatao 5 milioni wanakabiliwa na matatizo ya kornea, sehemu ya mbele ya jicho iliyo ngumu na inayowezesha miale ya mwanga kupenya.

China watu milioni 5 wanamatatizo ya kornea lakini ni kornea 5,000 pekee ambazo hupatikana kila mwaka.

Matatizo ya konea husababisha watu wengi kuwa na ulemavu wa macho (upofu). Njia hiyo mpya ya kutibu upofu imeanza kutumiwa baada ya kuidhinishwa na serikali ya Uchina mwaka jana.

SOMA PIA:  Safaricom yapigwa faini ya mamilioni kwa sababu ya huduma mbovu

Kornea kutoka kwa Nguruwe hutibiwa na kutolewa bakteria na virusi, pamoja na kutolewa DNA ya Nguruwe, kabla ya kupandikizwa katika jicho la binadamu.

Wakosoaji wa mpango huo wanasema Uchina inaenda kwa kasi sana, bila kuangazia madhara ya mpango huo kwa kipindi kirefu.

Je wewe una mtazamo gani juu ya teknolojia hii ambayo pia inaweza wagusa watu wengine kiimani?

Chanzo: BBC Swahili

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com