Nigeria yaongoza kwa kuwa na watumiaji wengi zaidi wa Facebook barani Afrika

1
Sambaza

Nigeria inashikilia nafasi ya kwanza kwa kuwa na watu wengi zaidi wanaotumia mtando wa Facebook Afrika nzima.

Licha ya Nigeria kudorora kiuchumi lakini imeongoza kwa kuwa na watumiaji takribani milioni 16 wa Facebook. Kitendo cha Nigeria kuongoza kwa kuwa na watumiji wengi wa Facebook inamaanisha kuwa matumizi ya intaneti ni makubwa nchini humo.

Mwaka jana Afrika Kusini iliongoza kwa kuwa na watumiaji milioni 12 wa Facebook ikifuatiwa na Kenya (mil. 4.5). Nigeria inawatumiaji wa kila siku wa Facebook milioni 7.2 huku asilimia 97 kati ya hao wakitumia simu kuingia Facebbok.

Mbali na Nigeria kuwa kinara kwa kuwa na watu wengi zaidi wanatumia Facebbok pia nchi hiyo inaongoza kwa kuwa na idadi kuwa ya watu wanatumia simu janja na idadi hiyo inategemea kufikia milioni 95 ifikapo mwaka 2019.

Nigeria ikiwa na idadi kubwa zaidi ya watu wanaotumia Facebook.

Nigeria ikiwa na idadi kubwa zaidi ya watu wanaotumia Facebook.

Nchi ambazo hutumia simu kuingia Facebook kwa kutumia simu janja

Afrika Kusini kwa Madiba ndio inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wanaotumia simu kuingia Facebook ikiongoza kwa 34%, Nigeria (27%), Senegal na Kenya wote wakiwa na 15%, wakifuatiwa na Ghana (14%) huku Tanzania (8%).

country-ng-age-ratio

Uwiano wa kiumri nchin Nigeria katika matumizi ya mtandao wa Facebook.

Facebook yahusika katika kukuza kipato cha mtu mmoja mmoja

Watu wengi hasa nchini Nigeria wameweza kukuza vipato vyao vya kila siku kwa kutumia mtandao wa Facebook kutangaza bidhaa zao wakitumia simu janja kuingia katika mtandao huo na kutangaza biashara zao na kuweza kukuza soko la bidhaa zao ndani na je ya Afrika kwa kutumia Facebook.

SOMA PIA:  Skype yaingia mkataba na Paypal; sasa watumiaji wataweza kutuma pesa.

Licha ya Nigeria kuwa na idadi kubwa ya watu wanatumia Facebook lakini imekuwa ni tofauti kwa upande wa mapato yatokanayo na Facebook. Amerika Kask inaongoza kwa kuigiza dola mil. 13.52. Afrika na sehemu nyingine duniani inaingiza dola mil.1.22.

Vyanzo: Quartz Africa, BBC, mitandao mbalimbali

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com