Nile X: Simu janja ya kwanza kutengenezwa Misri yazinduliwa

0
Sambaza

Muongo mmoja uliopita tumeshuhudia ukuaji wa teknolojia ya simu za mkononi ikiruka kwa kasi ya mlipuko unaoendelea kukua na kudhihiri mapinduzi ya aina yake katika sekta ya simu janja.

Kadhalika soko la simu janja limeendelea nalo kukua kwa kasi kama ilivyo teknolojia ya simu zinazozalishwa
duniani kwa sasa. Lakini uzalishaji wa simu janja umekuwa ukitegemewa kwa nchi za bara la Ulaya, Amerika na Asia.

Bara la Afrika limekuwa mnunuzi na mtumiaji wa kinachozalishwa katika mabara hayo. Lakini hilo kwa sasa limekwisha. Nchi ya Bara la Afrika kwa mara ya kwanza imepata uzalishaji wa simu janja yake yenyewe
kwa mara ya kwanza.

NILE X

Muonekano wa simu ya Nile X

Nchi ya misri (Egpty) kupitia kampuni yake ya Silicon Industries CO (SICO) wiki mbili zilizopita ilizindua simu janja inayoitwa Nile X katika mji wake mkuu wa Cairo.

SOMA PIA:  Alpha One: Simu janja ya bei ghali kutoka familia ya Lamborghini

Katika sherehe za uzinduzi wa Nile X Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa Misri Mhandisi Yasser El Kady alisema wamefurahi kutimiza malengo waliojiweke na Rais wa nchi hiyo Abdel Fattah El Sisi alipewa kama zawadi na kuwa mtumiaji wa kwanza wa simu hiyo.

Katika kusukuma sekta ya teknolojia, uongozi wa Rais El Sisi umeipa sapoti kubwa kampuni ya SICO katika kufanikisha azma hiyo ya kuunda simu.

Kiwanda cha utengenezaji wa simu cha SICO kimegharimu kiasi cha Dola za kimarekani milioni 22.5 kwa uwekezaji uliowekwa katika mji wa Assiut.

SOMA PIA:  Mapendekezo ya Apple kuhusu kuja na emoji zinazohusu walemavu

Misri inawatumiaji wa simu waliosajiliwa zaidi ya asilimia 98 katika watu milioni 95 wa nchi ya hiyo. Simu hiyo imeanza kuuzwa Desemba 15 nchini Misri na inatarajiwa kuuzwa baadae kati nchi zingine za Afrika.

nile x

Asilimia 55 ya vifaa vyote vinavyotumika katika utengenezaji huo vinatengenezwa hapo hapo Misri wakati malighafi zingine zinanunuliwa kutoka China.

Pia kampuni ya SICO inataraji kufungua masoko katika ukanda wa Afrika mashariki hususani katika mji wa Nairobi, Kenya, Msumbiji, Afrika Kusini na Nigeria.

Simu ya Nile X itaendeshwa kwa mfumo maarufu wa Android toleo la Nougat pamoja na Prosesa ya
Octa Core, ambapo ukubwa wa kioo cha simu hiyo utakuwa inchi 5.7 HD.

SOMA PIA:  Undani wa Nokia 8 na kupata masasisho ya Android 8.0

Katika upande wa kamera zitakuwa mbili zenye megapixel 13 kwa kamera ya nyuma na mbele (selfie) itakuwa na megapixel 8.

Kwenye ukubwa wa uhifadhi wa ndani(Storage) itakuwa na GB 64 pamoja na RAM ya ukubwa GB 4. Simu hiyo itakayo kuwa na teknolojia ya 4G, sensa ya kidole(Fingerprint sensor) pia itaruhusu mfumo wa kuchaji kwa haraka(Fast charging) wa USB Type-C.

Ukubwa wa Betri ni 2800mAh pia ina sehemu mbili ya kuwekea Laini za simu. Nile X inatarajiwa kuuzwa kwa Dola 112 (Takribani Tsh 250,000/=) na matarajio kusambaza simu milioni 1.8 baada ya uzinduzi wake.

Vipi je una maoni gani juu ya simu hii?

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com