Njia Hizi Zitaongeza Ujazo Wa Uhifadhi (Memori) Katika Simu Yako Ya Android! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Njia Hizi Zitaongeza Ujazo Wa Uhifadhi (Memori) Katika Simu Yako Ya Android!

0
Sambaza

Ukiachana na jinsi ya kuongeza ujazo wa uhifadhi katika simu za Android, hapo nyuma tuliandika kuhusiana na jinsi gani tunaweza tukaongeza ujazo katika simu za iPhone.

Kusoma juu ya kuwezesha hilo katika iPhone soma hapa

Simu zinazotumia program endeshaji ya Android ndizo zinazoongoza kutumiwa duniani kote. Mara nyingi watu wanapata changamoto kwani vifaa hivyo huwa vinajaa mara kwa mara. Mambo yamekua mengi sana siku hizi na yote yanahitaji nafasi katika vifaa vyetu

get link Tuzifahamu Njia Hizo

http://fophs.org/president-messsage/our-march-2013-newsletter/ 1. Futa App Za Zamani Na Zile Ambazo Huzitumii

Kuna uwezekano mkubwa sana kwamba App zetu zinatumia ujazo wa uhifadhi mwingi sana katika vifaa vyetu vya Android. Hapa cha msingi ni kuweza kufuta App hizo zote ambazo ni za zamani na ambazo mtu hazitumii kwa wakati huo. Hii inatokwa mara nyingi, utakuta mtu alishusha mchezo (gemu) na baadae akalichoka lakini akawa hakulifuta. Hilo litakuwa ni moja kati ya mambo yanayojaza ujazo wa uhifadhi

INAYOHUSIANA  Nokia 7 Plus; Simu inayoiweka vizuri Nokia kwenye soko la ushindani

Kufuta App Nende katika – Settings

http://rockthehillsvt.com/event/snowbog-v/ – Ingia katika Applications au Apps
– Ingia katika App Ambayo unataka kufuta
– Na kisha Uninstall ili kuifuta

Jinsi Ya Kufuta App

2. Futa Mambo Uliyoyashusha (download) Ambayo Hayana Umuhimu Tena

Kama una tabia ya kushusha mambo mengi sana katika mitandao basi hii inakuhusu. Kumbuka sio wote wenye simu za Android kwenye vifaa vyao vina ile sehemu iliyoandikwa Downloads, ya kwako inaweza ikawa imeandikwa My Files au kitu kama hicho. Sehemu hizo ndio zinahifadhi mambo yote tunayoyashusha kama vile nyaraka mbali mbali, picha na kadhalika

Kufuta Vitu Hapo ingia katika – My Files au katika simu zingine ingia katika Downloads

– Ingia katika Downloads
– Chagua faili unalotaka kulifuta kwa kuligusa
– Baada ya hapo bonyeza katika kile kialama cha kufuta

Jinsi Ya Kufuta Mambo Mengine Uliyoyashusha

3. Futa Miziki
Hapa kidogo wengine wanaweza wakawa watata,sawa tunapenda miziki kwa kiasi kikubwa sana. Sema ngoja nikuulize swali. Je huwa unasikiliza miziki yote katika simu yako? Namaanisha YOTE? Au ndio kuna mingine huwa unaruka ruka? Kama ukiwa na jibu basi hiyo ambayo huwa unaruka ruka inabidi uifute ili kuongeza ujazo wa uhifadhi katika kifaa chako cha Android

Moja Ya Katika Ya Huduma Ya Muziki Wa KU'Stream' Kutoka Google Maarufu Kama 'Google Play Music'

Moja Ya Katika Ya Huduma Ya Muziki Wa KU’Stream’ Kutoka Google Maarufu Kama ‘Google Play Music’

Au ukitaka unaweza ukatumia huduma za muziki wa ku’stream’. Huduma hizi huwa hazily ujazo mwingi wa uhifadhi katika vifaa kama zile njia zetu za kawaida za kuhifadhi nyimbo

INAYOHUSIANA  Umoja wa Ulaya kudhibiti gharama za simu

4. Futa Video Zenye Ujazo Mkubwa

Ushawahi kuona mtu ana video nyingi katika simu yake kama vile kazi yake ni u’Director’? (haha!). kuna watu wana video nyingi sana katika simu zao. Kwa mfano mtu anaweza akawa na simu imejaa video nyingi sana za vichekesho, kumbuka kuna video nyingi sana za vichekesho na kamwe huwezi ukawa nazo zote. Kama video hizo zikiwa ni za muhimu sana basi huna budi kuzihamishia katika kompyuta na kisha ukafuta katika simu yako

5. Tumia Memori Kadi (MicroSD Card)

Kumbuka sio kila simu zote za Android zina uwezo wa kukubali memori kadi. Zingine zinakuja na ujazo wa ndani tuu. Kama wewe simu yako inaruhusu memori kadi basi huna budi kutafuta moja ambayo itakusaidia kuweka vitu vyako. Memori ziko za ujazo tofauti tofauti kulingana na mafaili yako tuu unayohifadhi.

INAYOHUSIANA  Apple kununua vioo vya simu kutoka LG badala ya Samsung

6. Tumia uhifadhi wa mtandaoni

Kama bado unaona ujazo hautoshi na una mambo mengi sana huna budi kuwa unatumia uhifadhi wa mtandaoni. Ili kuweza kuhifadhi mafaili yako (picha, miziki, video, nyaraka n.k) bofya hapa

Mambo haya machache yatakufanya uweze kushughulikia simu yako ya Android vizuri katika swala zima la ujazo wa uhifadhi. Kama una wazo au njia nyingine ningependa kusikia kutoka kwako. NIandikie hapo chini sehemu ya comment.

Tembelea TeknoKona kila siku ili kupata habari moto moto. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.