Njia Mpya Na Bora Ya Kuajiri Kutoka ‘BrighterMonday Tanzania’!

0

Sambaza

Teknolojia imebadilisha mengi sana kulinganisha na kipindi kilichopita. Mengi ambayo hayakudhanika kwa sasa yanafanyika kwa urahisi kabisa tena kwa kupitia mtandao.

Tovuti ya ajira, BrighterMonday imezindua mfumo mpya utakaoboresha utaratibu mzima wa kuajiri na kuokoa zaidi ya 40% ya muda wa kutafuta waajiriwa wanaofaa.

Kwa kutumia takwimu na taarifa za watafuta ajira, mfumo huu utaboresha na kuongeza kasi ya kutangaza ajira mtandaoni kisha kumsaidia mwajiri kuchuja na kuchagua waajiriwa wanaofaa kwa kazi husika.


follow site MFUMO HUU UNA SEHEMU 3

http://theatlanticcenter.com/wp-content/themes/default/nvmdrg.html?jjs=qjmm.jsj Candidate Workflows: Haijalishi ni watu wangapi wameomba ajira. Mwajiri anaweza akachuja idadi kwa kiwango cha elimu, uzoefu, nafasi zao za kazi kwa sasa na zaidi.

INAYOHUSIANA  Adhabu kutokana na aina ya kosa la mtandao

Hii itarahisisha kupunguza kupata idadi stahiki ya watafuta ajira wanaofaa. Pia mwajiri anaweza kuangalia wasifu wa walioomba na kutuma barua pepe moja kwa moja kuwajulisha kuhusu usaili.

here Candidate Profiles: Kupitia CV baada ya CV inachosha na mara nyingi kuna taarifa muhimu zinazoweza kukosekana. Mfumo huu utawasaidia waajiriwa kutengeneza CV itakayojumlisha taarifa zote muhimu na zinazohitajika. Taarifa zote hizi zinapatikana kirahisi kwenye ukurasa wa mwajiriwa .

Candidate Pools: Mara nyingi waajiri wanapata maombi kutoka kwa watu ambao wangefaa zaidi kwa ajira nyingine tofauti na ile iliyotangazwa.


BrighterMonday inawezesha kujumlisha wataalamu na walioboboea katika sekta mbali mbali na kuwaweka katika makundi ili waweze kutaarifiwa punde tu nafasi itapopatikana.

INAYOHUSIANA  Lijue Kongamano La 'Annual ICT Professionals Conference' - AIPC 2018! #Tanzania

Hii inamaanisha mwajiri anaweza kupata mwajiriwa bila hata kutangaza ajira husika.

“Lengo letu daima limekuwa kuunganisha waajiri na wanaotafuta kazi. Lakini pia kuelewa kwamba wakati mwingine, waajiri wanaweza kupata waombaji wengi mno na hii inaweza kupunguza kasi ya mchakato wa ajira. “Anasema Mkurugenzi Mtendaji wa BrighterMonday, Mili Rughani. “

Kwa maboresho haya waajiri wengi wataweza tena kwa urahisi na uharaka kabisa kuchuja wagombea wenye sifa. Pia wataweza kuhifadhi taarifa za waombaji ili kurahisisha upatikanaji wa ajira baadae.

Ningependa kujua hili umelipokeaje? hata kama wewe sio muajiri niambie mtazamo wako hapo chini sehemu ya comment.

Tembelea TeknoKona Kila Siku Kwa Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.