Njia rahisi ya kujua sifa ya Kompyuta yako (uwezo wake)

0
Sambaza

Kuna mazoea ya kutumia kitu kwa muda mrefu bila ya kujua wasifu wake halisi. Hili linapatikana sana miongoni mwetu.

Mfano kuna mtu ni dereva wa gari wa muda mrefu lakini akiulizwa sifa ya gari anayoiendesha huwa haijui. Au Kompyuta ambayo ipo ofisini kwake au nyumbani aitumiayo kila siku, lakini hajui wasifu wake vizuri.

Leo tutakuelekeza namna ya kujua sifa za kompyuta yako ambayo umekuwa ukiitumia kila siku. Namna ya kupata maelezo ya Kompyuta yako kuna njia tutakuelekeza ambazo kila mmoja ataweza kujua.

SOMA PIA:  Apps mbalimbali katika simu moja kwa akaunti mbilimbili

Njia rahisi ya kujua sifa ya Kompyuta yako: Njia hii ni kwa Kompyuta zinazotumia mfumo wa Windows na Mac.

Kwa wanaotumia kompyuta za Mac, unachotakiwa ni kubonyeza Icon ya Apple iliyopo juu upande wa kushoto kisha bonyeza About This Mac.

Njia rahisi ya kujua sifa ya Kompyuta yako

Mfumo wa Windows

Kwa wale wanaotumia Kompyuta za Windows unabonyeza Win na R kisha utaandika msinfo32 katika search bar na halafu bonyeza OK.

Mpaka hapo utakuwa umejua jina halisi la Kompyuta yako na sifa zake kadhaa. Jaribu nawe utuambie Sifa ya Kompyuta yako.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com