Nokia 3310 kuja upya: Je upo tayari kuitumia tena?

1
Sambaza

Kabla iPhone haijaja na kubadili soko, kabla simu za Android hazijaja na kuliteka soko…..Nokia ilikuwa haina mpinzani katika utengenezaji na uuzaji wa simu duniani kote, na simu ya Nokia 3310 ilikuwa moja ya simu maarufu zaidi kutoka kwao.

Soma pia – Hizi Ndizo Simu 20 Zilizouzika Zaidi Duniani Hadi Sasa! – TeknoKona

Habari njema ni kwamba muda si mrefu simu hiyo itaweza kupatikana tena kwa wingi zaidi. Kampuni ya HMD Global inayoshikilia haki miliki za utumiaji wa jina la Nokia imesema inakuja na maboresho kidogo ila ikiwa inahakikisha muonekano unabadikia ule ule, simu ya Nokia 3310 inakuja tena sokoni.

Simu ya Nokia 3310

Simu ya Nokia 3310

Simu hiyo iliingia sokoni kwa mara ya kwanza mwaka 2000, enzi hizo ikiwa na sifa kuu ya upigaji simu, sms, calculator, magemu kama vile Snake II na miito ya simu (ringtones) saba. Kwa kifupi sifa zake ni za kawaida sana ukilinganisha na simu za sasa hivi.

SOMA PIA:  Google waliuza simu za Pixel takribani milioni 4 mwaka 2017

Sifa kuu ya Nokia 3310 ni uwezo wa kuvumilia mengi, hauutaji kuichaji kila siku na unaweza irusha umbali mrefu tuu na ikatua bila ata ya kuharibika.

Bei ya simu hiyo inategemewa kuwa dola 63 za kimarekani, ambayo ni takribani Tsh 130,000/=.

Tunategemea kutakuwa na maboresho kadhaa watakayokuwa wameyafanya hasa hasa kwenye programu endeshaji itakayotumika.

Soma pia – Hizi Ndizo Simu 20 Zilizouzika Zaidi Duniani Hadi Sasa! – TeknoKona

Tutaendelea kufuatilia, simu inategemewa kutambulishwa ndani ya wiki chache hizi.

SOMA PIA:  Apps zilizopakuliwa mara nyingi zaidi tangu kutambulishwa kwake #Uchambuzi

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com