Sote tunafahamu jinsi simu Nokia 3310 ilivyokuwa maarufu miaka ya mwanzo ya 2000 na kuifanya kampuni ya Nokia kuwika sana katika miaka hiyo kutokana na simu hizo kuwa imara sana na zinazodumu na chaji kwa muda mrefu.
Kutokana na ukuaji wa teknolojia na simu janja kwa ujumla Nokia wakaona si vibaya iwapo wakirudisha simu yao iliyotokea kupendwa na wengi sehemu nyingi duniani lakini ikiwa na upya unaoendana na mahitaji ya wateja (intaneti, umbo/ukubwa, uimara, n.k) na hapo ndio mapema mwaka huu (2017) Nokia wakatambulisha NOKIA 3310 ya kijanja zaidi.
Yaliyoboreshwa kwenye toleo jipya la Nokia 3310
Kiujumla katika toleo jipya la Nokia 3310 hakuna kipya kilichoongezwa isipokuwa tu ni kuboresha yale yaliyopo kwenye toleo lililopita na kuifanya kuwa simu janja ambayo itatokea kupendwa tena na kuweza kuifanya Nokia ifanye vizuri katika soko la simu jaja. Uchambuzi wa yaliyoboreshwa kwenye Nokia 3310 ni kama ifuatavyo:-
>Teknolojia ya 3G/Uwezo wa betri
Katika toleo lilipita simu ya Nokia 3310 (lililotoka mapema mwaka huu) lilikuwa linakubali teknolojia ya 2G na 3G ila katika toleo la hivi sasa simu hizo zinakuja zikiwa na teknolojia ya 3G pekee tofauti na hapo awali.
Ni wazi kuwa simu yoyote inayotumia teknolojia ya 3G au zaidi inatumia kiasi kikubwa cha chaji lakini kwenye toleo jipya la Nokia 3310 umbo la betri halijabadilishwa/kuboresha igawa kikubwa zaidi kwenye tole jipya la Nokia 3310 ni kwamba betri katika toleo jipya la simu hizo linadumu na chaji kwa muda wa saa sita na nusu (kwa kuongea) tofauti na hapo awali kwenye toleo lililopita ambapo betri lake linadumu na chaji kwa saa 22 kwa kuongea.
>Umbo na rangi za simu
Imewekwa wazi kuwa katika toleo jipya la Nokia 3310 simu hizo ni ndefu kidogo kuzidi toleo lililopita, nyembamba na nyepesi zaidi. Rangi zake ni nyekundu, bluu, njano na nyeusi.
>Bei/Programu endeshi
Bei ya kitu chochote ndio moja ya kiutio cha mteja kuweza kununua bidhaa husika na vivyo hivyo kwenye toleo jipya la Nokia 3310 bei yake imeongezeka na kufikia karibu $81|Tsh. 182,169 huku simu zilizopita zikiuzwa kwa $58|Tsh. 130,442 (bei zote ni kwa Marekani).
Kwa simu janja yoyote ile ni lazima iwe inaendeshwa kwa programu endeshi, hata hivyo haijawekwa wazi ni maboresho gani yalipo kwenye toleo jipya la Nokia 3310 kwa upande wa programu endeshi ingawa imeelezwa kuwa mtumiaji ataweza kuhisi tofauti ya programu endeshi kwenye toleo lililopita na toleo la hivi sasa.
Simu hizo zimeanza kuuzwa nchini Marekani lakini zinatarajiwa kuanza kupatikana kwingineko duniani baadae mwezi huu. Je, umefurahia uamuzi wa Nokia kuachana na teknolojia ya 2G kwenye simu za Nokia 3310?
Vyanzo: The Verge, PCmag
One Comment
Comments are closed.