Nokia 6: Kuingia madukani mwezi Julai

0
Sambaza

Baada ya ukimya wa muda mrefu hatimaye simu ya kwanza ya Nokia ipo mbioni kutoka, hii ni  baada ya mkataba baina ya Nokia na Microsoft kuisha.

Mwanzoni mwaka huu kampuni  kutoka Finland inayojihusisha na utengenezaji wa simu za Nokia ilitangaza kutengeneza simu janja kadhaa zitakazotumia Android.

nokia 6

Nokia 6

Mtandao wa Nokia umetoa  taarifa zaidi juu ya Nokia 6 moja ya simu hizo ikiwa ni pamoja na kwamba itaingia dukani mwezi ujao.

SOMA PIA:  Google kutambulisha simu janja mbili mwezi Oktoba

Nokia 6 inakuja na kioo cha nchi 5.5 na kikiwa na uwezo wa HD, kamera ya nyuma yenye Megapixel 16 wakati ile ya mbele ina Megapixel 8. Simu hiyo pia inakuja na 3GB RAM wakati memori inakuwa na 32GB ambazo pia unaweza ongeza kwa kudumia memori kadi.

Simu hii inategemewa kuwa madukani mwezi Julai (nchini Marekani) na itakuwa inatumia OS ya Android Nougat ambayo ni OS ya kisasa kutoka Google. Simu hii imetengenezwa kuwa imara kwa kuzungushiwa ganda la aluminium na kuipa ubora zaidi, pia itakuja na katika matoleo mawili la laini moja na la laini mbili.

nokia 6

Muonekano wa nyuma.

Simu hii inategemewa kuanza kuuzwa katika Amazon nchini Marekani inakuja katika rangi nyeusi isiyong’aa na fedha. Tayari Nokia wametangaza kwamba wataleta simu nyingine ndogo zaidi ya Nokia 6 lakini hiajajulikana hasa ni lini zitaingia sokoni.

SOMA PIA:  Udanganyifu unaoweza kusababisa 'ukaibiwa kidigitali' wabainika kwenye bidhaa za Apple

Je ulishawahi tumia simu za Nokia? unategemea nini katika toleo la simu hizi linalokuja? tujulishe kwa kuandika maoni.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com