Nokia 8 Sirocco: Simu janja matata, yenye kava imara

Nokia 8 Sirocco: Simu janja matata, yenye kava imara

0
Sambaza

Kampuni HDM Global inayotengeneza simu za Nokia mwishoni mwa wiki iliyopita na siku moja kabla ya uzinduzi wa Mkutano wa Mobile World Congress huko Barcelona nchini Uhispania, ilitangaza kuzindua simu janja ya Android imara na ngumu zaidi duniani.

Simu hiyo inayotajwa kuwa ni ngumu kuvunjwa kwa mkono ni Nokia 8 Sirocco. Uzinduzi wa simu janja hii umeleta gumzo kubwa kwa wafuatiliaji wa mambo ya simu.

buy finasteride online malaysia Kikubwa kilichovutia simu hii ni muundo wa Kava ya yake kuwa katika muundo wa chuma. Simu janja nyingi zimekuwa zikitengenezwa bodi yake katika muundo wa malighafi ya Aluminium. Kava ya simu hii ni imara na ngumu zaidi ya mara mbili ya bodi ya simu za Aluminium.

INAYOHUSIANA  Huawei na simu ya kwanza yenye RAM GB 8

Muundo wa Kava ya simu ya Nokia 8 Sirocco unafanana na ule wa Simu ya Nokia 8800 iliyotoka 2005 ambayo Kava yake ilikuwa ya chuma cha pua.

Nokia 8800 ya mwaka 2005

Mbali na na kuwa na kava ya chuma pia asilimia 95 ya uso wa nje wa Nokia 8 Sirocco ni kioo. Na kioo chake kimepinda (Curves) kidogo mfano wa kioo kama cha Samsung. licha ya ugumu wa Bodi yake pia haiingi maji wala kusumbuliwa na vumbi.

http://abraxasgp.com/tag/emerging-markets/ Ukubwa wa kioo cha simu hii ni 5.5-inch chenye teknolojia ya P-OLED QHD (1440×2560). Kwenye upande wa Kamera itakuwa na kamera mbili za nyuma moja ina ukubwa wa 12MP na nyingine yenye 13MP zikiwa zimetengenezwa na kampuni ya kijerumani ya Zeiss. Kamera ya mbele (Selfie) itakuwa na uwezo wa 5MP na kuweza kurekodi video ya 1080p.

INAYOHUSIANA  Motorola wametoa nyingine inaitwa Moto Z3

Upande wa betri lina ujazo wa 3260 mAh ambapo chaji yake inaweza kukaa kwa siku moja hadi mbili kwa utumiaji wa kawaida.

Nokia 8 Sirocco

buy Lamictal without a prescription in the united states Sifa nyingine ya simu ni kama ifuatavyo:
Ukubwa wa RAM ni 6GB
Uhifadhi ni 128GB

Mawasiliano ni:
GSM: 850/900/1800/1900
CDMA One: BC (800)
CDMA 2000: BC0 (800)
WCDMA: 1,2,5,8,
TDS CDMA: 34,39
FDD-LTE: 1, 2, 3, 4, 5, 7, 8, 20, 28

Ulinzi
Fingerprint sensor

Mfumo endeshi:
Android Oreo

Nokia 8 Sirocco

Wachambuzi wa mambo ya simu wanaiona simu hii ni kama ya thamani sana na inaweza kuwa jibu sahihi kwa simu nyingi ambazo zimekuwa zikiharibika kava zake kwa haraka zaidi.

INAYOHUSIANA  Uganda: Sheria ya kodi ya mitandao ya kijamii kupitiwa upya

Hata hivyo kuna wasiwasi simu kuwa nzito kutokana na Kava lake kuwa la chuma hivyo kuleta shida hasa pale inapowekwa mfukoni na ikiwa kwenye Vibration kushindwa kutoa ishara nzuri ya mtikisiko wake.

Bado Nokia hawajaweka wazi uzito wa simu hiyo. Bado uzito hautakuwa shida sana bali simu inaonesha thamani ya pesa ya mteja. Kwa utoaji wa simu za namna hii HMD Global wanaonekana wamejiimarisha katika kurudisha kwenye chati jina la Nokia kwenye biashara ya simu.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.