Ndani ya mwaka huu (2017) tu Nokia imetoa simu sizizopungua tano katika hali ya kuifanya simu za Nokia zinarudi katika umaarufu wake iliyokuwa nayo zamani na kuleta ushindani kwa makampuni mengine.
Nokia 8 ni moja kati ya ule muendelezo wa simu za Nokia kutoka Nokia 1, 2, 3….mpaka 9 na wakati Nokia 8 inatoka haikuwa na toleo la Oreo (Android 8.0), toleo ambalo mpaka sasa si simu janja zote za Android zimepata sasisho hilo. Kwa wenye Nokia 8 ni wakati wa kufurahi kwani simu hizo sasa zinaweza kufanya masasisho na kuwa na Android 8.0.
Je, Nokia 8 ina sifa gani?
HMD Global ambao ndio watengenezaji wa simu za Nokia hivi sasa na Nokia 8 ina sifa nyingi za kuvutia simu hiyo jambo ambalo ni jema kabisa baada ya simu zake zilizokuwa zikitengenezwa na Microsoft kuifanya kampuni hiyo kuyumba kabisa kwenye biashara ya simu janja. Nokia 8 ilizinduliwa mwezi Agosti 2017 na kuanza kuuzwa duniani kote mwezi Oktoba 2017. Sifa za Nokia 8 ni kama ifuatavyo:-
1. Prosesa/Kioo.
Simu janja Nokia 8 ina moja ya prosesa za kisasa kabisa na zenye nguvu iitwayo Qualcomm Snapdragon 835 SoC ambapo kasi yake ya kufanya kazi ni mpaka 2.5 GHz Kryo na 4×1.8 GHz Kryo. Upande wa kioo kina ukubwa wa inchi 5.3 QHD na ikitokea akaidondosha Nokia 8 si rahisi kuvunjika kwa sababu inatumia teknolojia ya kisasa katika vioo vya simu janja nikimaanisha Corning Gorilla Glass 5.
2. Kamera/Diski uhifahi.
Nokia 8 ina kamera 2; kamera ya mbele (mahususi kwa selfie) na ile ya nyuma ila cha kuvutia kuhusu simu hii kwenye upande wa kamera ni kwamba zote zina ubora uleule picha kwa maana ya kwamba kamera ya mbele na nyuma zote zina MP 13.
Kwenye diski uhifadhi mtumiaji anaweza asiwe na haja ya kuweka ujazo wa ziada; Nokia 8 inakubali SD card ya mpaka GB 256 lakini ujazo wa kwenye simu janja Nokia 8 ni GB 64.
3. Utambuzi wa alama za vidole/Bei yake
Ulinzi madhubuti kwenye simu janja ni kipaombele katika makampuni mengi makubwa yanayojishughulisha na biashara ya simu janja na teknolojia ya utambuzi wa alama za vidole imeshika kasi kwa sasa na kwenye Nokia 8 teknolojia hii ipo sehemu ya mbele na si myuma kama simu nyingi za Android. Bei yake ni $715|Tsh. 1,608,750.
Sifa nyinginezo
Sifa |
Uwezo |
RAM | GB 4 (ya 64 GB diski uhifadhi) na 6 GB (ya GB 128 diski uhifadhi) |
Uwezo Wa Betri | Li-Ion 3090mAh ambalo haliwezi kutolewa ndani ya simu na linakaa na chaji kwa saa 78 |
Uwezo Wa Kioo | 1440×2560 pixels |
Laini za simu | Inakubali laini 2 |
Wembamba | 151.5×73.7×7.9mm |
Sehemu ya kuchomeka spika za masikioni | Ina ukubwa wa 3.5mm |
Rangi | Tempered Blue, Polished Blue, Steel, Polished Copper |
Network/Teknolojia nyinginezo | 4G VoLTE, Wi-Fi 802.11ac, Bluetooth v5.0, GPS/A-GPS, USB Type-C (v3.1), haina redio |
Sasisho la Oreo lina ukubwa wa MB 1518 hivyo ni vyema ukahakikisha kuwa una kifurushi cha kutosha kabla ya kuanza kuingiza sasisho hilo kwenye simu janja ya Android.
Vyanzo: Gadgets 360, GSMArena