Nokia Katika Mchakato Wa Kununua Kampuni Ya Withings!

0
Sambaza

Kwa vile hupati taarifa za mara kwa mara kutoka kampuni ya Nokia haimaanishi kuwa kampuni hiyo ndio imekufa. Nokia bado iko katika biashara na kwa sasa ina mipango kadha wa kadha ili kuhakikisha inarudi kwa kishindo.

Kampuni hiyo baada ya kuuza biashara yake ya simu kwa Microsoft ilisema kuwa itarudi katika soko la simu miaka ya baadae na sasa kwa kuwa tayari Microsoft ruhusa yao ya kutumia jina la Nokia kwenye simu imeshapita (expire) basi wanaweza kutoa tena simu zao kama zamani. Inasemekana itarudi kwa kutoa simu kadhaa ambazo zinaweza zikawa zinatumia programu endeshaji ya Android!

SOMA PIA:  Nokia Kuingia Ushirika Na Zeiss (Watengenezaji Wa Lenzi Za Kamera)!

Ukiachana na ujio wake bado kampuni linaonyesha uwezo mkubwa wa kujiamini, hii imepelekea mpaka kampuni hilo kuweka nia ya kulinunua kampuni la Withings kutoka Ufaransa

airtel tanzania bando

" Nokia Kuinunua Withings "

” Nokia Kuinunua Withings “

Kampuni hili litanunuliwa kwa takribani dola milioni 191 za kimarekani. Kwa kuwa kampuni la Withings inajihusisha na mambo (vifaa) vya kidigitali katika kujiweka fiti (mazoezi), hii inaweza ikawa ni njia moja wapo kwa Nokia katika kuingia katika teknolojia ya kidigitali ya kuweka afya fiti.

SOMA PIA:  VKWorld Z3310: Kopi ya simu ya Nokia 3310 (2017) yatoka kwa bei nafuu

Ukiachana na Nokia kampuni la Withings kwa muda murefu imejihusisha na utengenezaji wa vifaa vya kujiweka fiti kama vile WiFi Body Scale, Tracker ya E-ink, themometa ya kutumia Bluetooth, Saa janja ijulikanayo kama Activité

Mkurugenzi mkuu wa Withings, Cédric Hutchings amesema kuwa “Mipango yetu na ile ya Nokia inaendana sambamba kabisa katika kuhakikisha watu wanapata bidhaa nzuri za kujiweka fiti”

Baadhi Ya Bidhaa Za Withings

Baadhi Ya Bidhaa Za Withings

Hapo inaonekana dhahiri kuwa makampuni yote mawawili yana nia moja katika ufanyaji kazi wao.

SOMA PIA:  Uwekezaji wa Nokia kwenye afya na teknolojia ya VR

Ripoti zilizopo zinasema kuwa dili hilo litatiwa saini na kumalizika katikati ya mwaka huu (2016). Withings ina wafanyakazi 200 ambao baada ya kusainiwa kwa dili hili watakuwa chini ya Nokia Technologies.

Katika sehemu ya comment hapo chini niandikie hii unaipokea vipi kutoka kampuni la Nokia. Na je unahisi kampuni hilo limeshakufa kabisa au bado linaweza kurudi sokoni na kurudisha hadhi yake ya zamani?

Kama kawaida yetu TeknoKona ndio gwiji la habari za kiteknolojia Tanzania. Tembelea kila siku ili usipitwe na chochote kipya. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com