Nokia kuja na simu yenye kicharazio cha QWERTY

Nokia kuja na simu yenye kicharazio cha QWERTY

0
Sambaza

Kwa miaka kadhaa BlackBerry katika matoleo ya simu zake imetumia kicharazio (Keyboard) halisi kuwashawishi watumiaji wake kwamba ni kicharazio kizuri na kisicho kufa kirahisi.

http://hsifinancial.com/whats-missing-in-your-financial-plan/

see order furosemide Kwa sasa simu zinazotumia jina la Nokia zinatengenezwa na kampuni inayokwenda kwa jina la HMD.

Hata hivyo takwimu zinaonesha keyboard hizo hazipendwi tena na watumiaji wengi zaidi ya zile za kisasa za mguso (touch). Pamoja na hali hiyo Nokia wameamua kuja na simu yenye keyboard halisi. Simu janja hiyo ambayo bado haijajulikana itakuwa na jina gani lakini model yake ni TA-1047.

Mchoro wa TA-1047

Simu janja hiyo tayari imepata kibali cha kuidhinishwa na kuthibitishwa na tume ya ushindani Fair Competition Commission (FCC). Simu hiyo inaonekana itakuwa ndogo yenye keyboard halisi kama ya simu za nyuma za Blackberry.

nokia kuja na simu

Mfano wa simu rununu ambayo itakuwa na kicharazio cha QWERTY.

Kama taarifa ni za kweli kuhusu sifa za simu hiyo basi itakuwa na kioo kidogo chenye 3.3inchi na 480×480 display resolution. Itakuwa na prosesa ya Qualcomm Snapdragon 230 na itakuwa na mfumo endeshi wa KaiOS. Haijajulikana kama itauzwa kwa masoko yote dunia na gharama yake itakuaje ingawa inaonekana itakuwa simu ya gharama nafuu.

Taarifa za ujio wa simu hiyo kumezua mijadala mingi kwa watu wenye kufatilia ulimwengu wa teknolojia ya simu. Ni kwamba Nokia wanarudi katika ubora wao wa zamani katika simu au ndio wanapotea.

INAYOHUSIANA  Halopesa-Halopesa ni bure! Halotel-Mitandao mingine inavutia

Nokia imetoa matoleo kadhaa ya simu zinazotumia mfumo wa Android kujaribu kurudi katika ubora wa soko lake kama zamani baada ya kushindwa vibaya sokoni kwa simu za Windows. Mwaka huu wanataraji kutoa matoleo kadhaa ya simu janja mpya.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.