Nokia kuja na simu za kupinda ‘foldable’, hadi eneo la display/screen – wachukua hakimiliki ya teknolojia

1
Sambaza

Kuna uwezekano mkubwa Nokia kuja na simu inayoweza kupinda kioo ‘screen’ kati kati, na hivyo simu ikawa na uwezo wa kukunjwa kati kati.

Jinsi simu itaweza kukunjwa

Hakimiliki ya teknolojia hiyo imegundulika katika taarifa za maombi ya hakimiliki yaliyotumwa na kampuni ya Nokia kwa chombo cha usimamizi wa masuala ya hakimiliki za kiteknolojia – yaani patents, cha nchini Marekani.

Teknolojia za display zenye uwezo wa kupinda imeshafikia sehemu kubwa na inategemewa muda si mrefu tutaweza kuona simu zinazokuja na uwezo wa kupinda ata eneo lenye display.

SOMA PIA:  Uwezo wa kurudisha kile kilichokuwa kimehifadhiwa kwenye memori ya simu

Makampuni yanayotegemewa pia kuja na simu hizo ni pamoja na Samsung, LG na ata Google. Vyombo vya habari kadhaa mwaka jana viliripoti juu ya mkataba kati ya LG na Google ambao utawawezesha Google kununua display/screen za simu kutoka LG zenye uwezo wa kupinda.

Angalia picha zinazoonesha hakimiliki ya teknolojia iliyoelezewa na Nokia.

nokia kuja na simu

Nokia kupitia ushirikiano wao na kampuni ya HMD Global walitambulisha simu yao ya kwanza inayotumia Android mwezi uliopita, Nokia 6. Ila simu hiyo kwa sasa itauzika nchini China tuu, ila muda wowote kuanzia sasa tutegemee tambulisho la simu nyingine kwa ajili ya soko la duniani kote.

Simu ya Nokia 6 – Kupatikana China tuu. Bei: Chini ya laki nne | Sifa: Android 7, Inchi 5.5 HD , RAM GB 4, Ujazo GB 64, | Snapdragon 430 processor | Kamera MP 16 – Selfi MP 8 |

Ingawa si mara zote upatikanaji wa hakimiliki ya mfumo bidhaa huwa unafanya makampuni husika kutoa bidhaa ila kwa kiasi kikubwa kuna uwezekano mkubwa Nokia wakajaribu hili kama sio mwaka huu basi hivi karibuni – vyanzo mbalimbali vimeripoti.

SOMA PIA:  Mwaka 2017 ulikuwa mwaka salama zaidi kwa safari za anga

Je unaonaje teknolojia hii ikija katika simu?

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com