Nokia matatani kwa wizi wa teknolojia!

1
Sambaza

Ile kampuni iliyokuwa haina mpinzani katika masuala ya teknolojia ya simu katika miaka ya 2000 na kurudi nyuma imejikuta matatani baada ya kufunguliwa kesi na Blackberry kwa tuhuma za wizi wa teknolojia.

Kampuni ya simu ya Blackberry inaishtaki Nokia kuhusu madai kwamba kampuni hiyo ya Finland imetumia uvumbuzi wake bila ruhusa. Madai hayo ya ukiukaji yanahusisha teknolojia inayotumika katika 4G pamoja na mitandao mingine ya simu.

Kampuni hiyo ya Canada inadai kwamba transmita za Nokia pamoja na programu nyingime zinatumia teknolojia yake. Blackberry inataka kulipwa fedha badala ya kuizuia Nokia kutumia teknolojia yake.

Mwaka 2012 Blackberry na Nokia zilizozana wakati Nokia ilipojaribu kuhakikisha kuwa mauzo ya simu za Blackberry yanapigwa marufuku nchini Marekani na Uingereza katika mzozo mwengine.

Blackberry inadai kwamba Nokia ilikuwa inajua uwepo wa uvumbuzi huo baada ya kujaribu kuununua hapo awali kabla ya Blackberry kuamua kutumia. Hili linaweza likaa ni doa kwa Nokia ukizingatia wanajiandaa kutoa simu aina ya Nokia 3310 iliyotamba miaka ya 2000.

Blackbery na Nokia wamesitisha utengenezaji wa simu zao na badala yake wametoa leseni za haki ya umiliki wa simu zao kwa kwa watengenezaji wengine wa simu. Je, unadhani Nokia wataweza kuepukana na kupatikana na hatia ya wizi wa teknolojia?

Vyanzo: BBC, TheGlobeAndMail

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
SOMA PIA:  Samsung Galaxy X kuwa simu ya kwanza yenye kioo chenye kujikunja na kujikunjua? #Uchambuzi
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com