Nusu ya watumiaji wa intaneti wanatumia pia mtandao wa Facebook!

Nusu ya watumiaji wa intaneti wanatumia pia mtandao wa Facebook!

0
Sambaza

Katika taarifa yao ya mapato waliyoitoa jana Facebook wametoa pia data zinazohusu utumiaji wa mtandao huo mkubwa duniani. Kufikia Novemba 2 tovuti hiyo imekuwa na wastani wa watumiaji bilioni 1.79 kila mwezi.

http://sanchezwindowcleaning.com/?page_id=227

watoto facebook
Watumiaji hawa ni wale ambao uingia katika tovuti hiyo angalau mara moja kila mwezi. Idadi hii ya bilioni 1.79, ni ukuaji wa asilimia 16 ukilinganishwa na wakati kama huu mwaka jana.
Tovuti inayojihusisha na data za kuhusu watumiaji intaneti duniani kote, Internet Live Stats, imekadilia ya kwamba kuna takribansi watumiaji bilioni 3.42 wa intaneti kufikia mwezi Julai mwaka 2016. Data za Facebook zinamaanisha takribani asilimia 52 ya watumiaji wote wa intaneti duniani wana akaunti kwenye mtandao wa Facebook (na wanafungua akaunti zao angalau mara moja kila mwezi).
watumiaji wa intaneti

Data inayoonesha ukuaji wa idadi ya watumiaji wa intaneti ikilinganishwa na asilimia ya watumiaji mtandao wa Facebook.

follow url Ukuaji wa watumiaji wa Facebook unauweka mtandao huo katika nafasi nzuri zaidi kibiashara. Tayari wanaingia mabilioni ya dola za kimarekani kila mwezi kutokana na matangazo yanayowekwa kwa watumiaji wake.
Ukuaji wa watumiaji wa huduma ya intaneti hasa hasa katika mataifa yanayoendelea kuna maanisha idadi ya watumiaji intaneti na wanaojiunga katika mtandao wa Facebook itaendelea kukua.

Tuambie una maoni gani juu ya ukuaji wa mtandao wa Facebook na utumiaji wa intaneti nchini?

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Kodi ya mitandao: Kampuni za simu kuzuia VPN nchini Uganda
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.