Nywila za mamilioni ya watumiaji wa Twitter zawekwa hadharani - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Nywila za mamilioni ya watumiaji wa Twitter zawekwa hadharani

0
Sambaza

Nywila za mamilioni ya watumiaji wa mtandao wa Twitter zimewekwa hadharani katika soko haramu mtandaoni zikiwa na majina wanayotumia watumiaji hao.

http://beltchenko.com/the-kokopellis-trail-trip-report/embed/

http://islam101.ca/lessons-from-eid-ul-adha/ Inakadiliwa kwamba nywila za mamilioni ya watumiaji wa Twitter zimewekwa katika soko haramu mtandaoni ambako zinauzwa kwa wale wanaozitaka, hili ni pigo jingine kwa mtandao wa Twitter ukiwa ni muendelezo wa mashambulizi na udukuzi ambayo yamekuwa yakitokea kwa siku za hivi karibuni.

Ingawa Twitter na vyanzo vingine vinasema kwamba nywila na majina hayo hayajapatikana baada ya mtandao huu kudukuliwa bali baada ya wadukuzi kudukua kompyuta za watumiaji.

Nywila

Twitter pamoja na vyanzo vingine wanakubaliana kwamba udukuzi huu haujafanyika katika server za Twitter, hii ni haari njema kwa Twitter kwasababu kama udukuzi ungefanyika katika server zao ingeshusha hali ya usalama wa server za mtandao huu.

INAYOHUSIANA  VIdeo za makundi kwenye Instagram sasa ni rasmi

> Je wadukuzi walipataje taarifa za watu wengi hivi?

Bado haipo wazi saana ni kwanamna gani wadukuzi waliweza kupata hizi taarifa ila inaaminika na wengi kwamba wadukuzi hawa walitumia aina ya fulani ya virusi ambayo ikiingia katika kompyuta ya mtumiaji huweza kuchukua taarifa za mitandao anayoingia na taarifa zake muhimu za kuingilia katika mitandao hiyo.

> Twitter wamefanya nini baada ya tukio hili?

Mtandao wa Twitter umezifunga akaunti zote pamoja na kuwaandikia barua pepe kuwaonya wamiliki wa akaunti zote ambazo taarifa zake zimewekwa katika mtandao na wadukuzi hao, hivyo watumiaji ambao ni waathirika wa shambulio hili watahitaji kupitia hatua fulani kurudiaha akaunti zao katika hali ya kawaida.

http://growingwell.org/deaconess-dental-at-western-hillsdater/student-6/ Tufanye nini ili tuwe salama? – Soma Pia, akaunti za mitandao ya kijamii ya muanzilishi wa Facebook yadukuliwa

Wataalamu wa mambo wanasema pamoja na mambo mengine tunatakiwa kuhakikisha kwamba tunatumia nywila na usernames tofauti kaikta kila mtandao, mmiliki wa Facebook kwa mfano akaunti yake ya twitter ilidukuliwa lakini inasemekana kwamba taarifa za mkuu huyu wa mtandao wa Facebook zilikuwa zinafanana na taarifa ambazo alizitumia katika mtandao wa Pinterest ambao ulidukuliwa huko miaka ya nyuma.

Makala hii imeandikwa kwa msaada wa mitandao ya habari mbalimbali ambayo iliandika habari hii kama vile The Telegraph.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

Comments are closed.