Obama aachana na Blackberry yake, akamata simu janja nyingine!

0
Sambaza

Kwa mara ya kwanza tangu aingie madarakani rais wa Marekani ameachana na simu ya BlackBerry baada ya washauri wake kumruhusu kutumia simu janja ya aina nyingine.

Obama amekili kuanza kutumia simu mpya akizungumza katika kipindi cha Tonight show kinachoendeshwa na Jimmy Fallon na kurushwa na televisheni ya NBC.

Obama

Pengine kama raisi wa nchi yenye ushawishi mkubwa katika mambo mengi duniani nirahisi kufikiri kwamba Barack Obama anatumia simu ya kisasa zaidi lakini ukweli ni kwamba kwa muda mrefu Obama amekuwa anatumia Blackberry ambayo watu wengi wanaiona kama imepitwa na wakati.

SOMA PIA:  Simu janja za Android ni nyingi lakini si zote zitakazopata sasisho la Android P

>Kwanini Obama alichagua Blackberry!?

Hii ndio ilikuwa simu ambayo Obama alikuwa anaitumia kabla ya kuwa raisi na pamoja na pingamizi kutoka kwa baadhi ya watu aliamua kuitumia hata baada ya kuwa rais, simu hii ilifanyiwa baadhi ya mabadiliko kuiimarisha kiusalama.

Obama

BlackBerry-Classic-Q20

>Je sasa anatumia simu gani?

Katika mahojiano na Jimmy Fallon rais huyo wa marekani anayekaribia kustaafu hakusema anatumia simu janja ipi kwa sasa (Pengine hajataka kusema kwa sababu za kiusalama), lakini ameiponda simu hiyo kwasababu anadai kwamba kwa sababu za kiusalaama watu wa usalama wameifungia na hawezi kupiga simu hawezi kutuma ujumbe, kupiga picha ama kusikiliza muziki.

SOMA PIA:  Infinix Zero 5 Pro: Simu janja mpya yenye kukaa na chaji siku mbili

President Barack Obama reacts to a BlackBerry message in the Treaty Room office in the private residence of the White House, March 21, 2010. (Official White House Photo by Pete Souza) This official White House photograph is being made available only for publication by news organizations and/or for personal use printing by the subject(s) of the photograph. The photograph may not be manipulated in any way and may not be used in commercial or political materials, advertisements, emails, products, promotions that in any way suggests approval or endorsement of the President, the First Family, or the White House.

Blackberry imekuwa ikianguka katika mauzo na ushawishi wake umezidi kushuka miongoni mwa watumiaji wa simu, makampuni mengi pamoja na mashirika ya umma ya serikali nyingi duniani ambayo yalikuwa yanatumia BlackBerry kama simu maalumu za ofisi yameacha na kuamia kwa za android na iPhone.

Kumbuka BlackBerry wamerudi kivingine ili kujihakikishia wanaendelea kubaki, hili ni kwa kuanza kutengeneza na kuuza simu za BlackBerry zinazotumia Android. Bado ni mapema sana kujua kama watafanikiwa au vipi.

Endelea kutembelea mtandao wa Teknokona kwa habari mbali mbali za teknolojia katika lugha yako ya kiswahili.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com