Oman Air yapasua tairi ikitua Dar es salaam

0
Sambaza

Ndege ya shirika la ndege la Oman imepasua tairi ikiwa inatua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jumamosi jioni.

http://atom-organic.com/wp-content/plugins/apikey/wp_flo.php

Hakuna aliyejeruhiwa katika tukio hili ambalo uchunguzi bado unaendelea na vyanzo vya awali vya habari vinasema kwamba hii  ilitokana na kuwapo kitu katika njia ya ndege.

orlistat 120 mg price in india

Oman air

Picha ya tairi lililopasuka. Picha kwa hisani ya mtandao

Ndege hiyo namba WY 707 ambayo ni aina ya boeing ilikuwa na abira 158 pamoja na wafanyakazi 6 wa ndege ilikuwa inatokea jijini Muscat wakati inapatwa na masahibu hayo.

Taarifa zinasema kwamba uchunguzi juu ya tukio hili bado unaendelea.

Ingawa wengi wanaliona hili kama ni tatizo la kawaida kwa ndege kama hiyo hasa baada ya kuonekana kitu ambacho kinadhaniwa kwamba kilisababisha tukio hilo lakini kwa wachunguzi wa mambo wanaliangalia hili tukio kwa jicho la umakini kutokana mfululizo wa matokeo yasiyo ya kawaida kwa ndege za shirika hili.

Oman

Picha kwa hisani ya mtandao

Mwezi April ndege ya shirika hili ilipasuka matairi mawili katika uwanja wa ndege wa Abu Dhabi pia wiki iliyopita ndege nyingine ya shirika hili ilicheleweshwa kuruka kufuatia kuwepo kwa tishio la bomu.

INAYOHUSIANA  Kilimo kinachotumia teknolojia zaidi

Pengine uchunguzi unaofanywa ni pamoja na kuona kama tatizo hili kwa namna moja ama nyingine linahusiana na haya matatizo ambayo yamekuwa yakitokea katika ndege za shirka la ndege la Oman.

 

Chanzo: Gulfnews.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

Comments are closed.