Ondoa programu ya QuickTime kwenye kompyuta yako! #Usalama - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Ondoa programu ya QuickTime kwenye kompyuta yako! #Usalama

0
Sambaza

Kama umepakua programu ya QuickTime kutoka Apple kwenye kompyuta yako ya Windows unashauriwa kuiondoa mara moja.

Watafiti mbalimbali wa mambo ya kiusalama wa kimtandao wamegundua ni rahisi sana programu hiyo kutumika kuvamia data za kompyuta zako kwa sasa.

programu ya quicktime

Tayari Apple walishatangaza kuacha kutoa masasisho (updates) kwa programu yao hiyo ambayo mara nyingi ilikuwa inakuja moja kwa moja pale unapotaka kupakua programu ya iTunes.

Ingawa programu ya QuickTime bado inaendelea kuwa na uwezo wa kufanya kazi ila ina ubovu wa kiusalama (security vulnerabilities) ambao ni hatari kwa data zilizokwenye kompyuta yako.

Kama una programu hiyo fuata hatua hizi kuiondoa kwenye kompyuta yako;

INAYOHUSIANA  Kingo Root: Programu/App ya Kuroot Simu za Android na Windows

see Kwa watumiaji wa Windows 10:

  • Bofya ‘Start’.
  • Chagua “Settings.”
  • Chagua “System” na nenda eneo la “Apps and features.”
  • Tafuta QuickTime kwenye orodha na kisha bofya “Uninstall.”

http://diasaonline.com/project/maxima-seguridad/ Kwa watumiaji wa Windows 7:

  • Bofya ‘Start’.
  • Chagua “Control Panel.”
  • Chagua “Programs”  na kisha chagua na kubofya “Programs and features.”
  • Tafuta QuickTime kwenye orodha na kisha bofya “Uninstall.”

Inasemekana kwa sasa ni kwa kompyuta za Windows tuu, Apple wanaendelea kutoa masasisho ya programu hiyo kwa wale wanaotumia kwenye vifaa vyao kama vile kompyuta za Mac.

Ni muhimu kuhakikisha unakuwa na programu zinazopata masasisho (updates) mara kwa mara ili kuzidi kukuhakikishia usalama wa data zako. Endelea kutembelea TeknoKona

purchase diflucan over counter vyanzo: grahamcluley.com na mitandao mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.