Kampuni ya OnePlus ni kampuni ya simu janja ambayo ina simu janja za aina yake. Kama makampuni mengine yalivyo, simu hii pia inatoa simu nzuri ambazo zinapatikana kwa bei nafuu kulinganisha na zile za Samsung na iPhone.
Baada ya kupata umaarufu mkubwa kupitia simu zao za OnePlus 1 na OnePlus 3 kampuni imeweka wazi siku ambayo inatarajia kutoa toleo lake jingine. Ukiachana na uzinduzi huo pia kampuni imeweka wazi vitu ambavyo watumiaji wake inabidi wavitegemee katika simu hiyo.
OnePlus 5 inatarajiwa kuzinduliwa Juni mwaka huu (2017). Ukaichana na tamasha la kuzundua simu hiyo tuu kampuni itafanya matamsha mengine madodo madogo katika kuhakikisha kuwa inaitangaza sana simu hiyo.
Kupitia mtandao wa Twitter kampuni iliujuza ulimwengu juu ya siku ambayo simu itazinduliwa rasmi.
Are you prepared for the OnePlus 5? Focus on what matters and join our keynote live on June 20. https://t.co/uuWc1m3pz1 pic.twitter.com/KfbVfMyh00
— OnePlus (@oneplus) June 6, 2017
SIFA ZA OnePlus 5
Mpaka sasa hakuna sifa za uhakika zaidi kwakuwa kumekuwa na fununu nyingi juu ya sifa zake na vyanzo vingi vilikuwa vinatofautiana kwa taarifa.
Kwa harakaharaka ni kwamba OnePlus 5 itakuwa GB 6 za RAM na prosesa yake itakuwa ni ile ya Qualcomm Snapdragon 835
Uwezo wake wa betri utakuwa mAh 3,600. Kwa upande mwingine bado taarifa hazijatoka ili kujua kama simu itakuwa inasapoti kuchaji bila waya (Wireless Chariging) kama zimu nyingine maarufu zilivyo.
Kwa upande wa umbo kampuni imeweka wazi kuwa simu hiyo itakuwa ni simu yao nyembamba zaidi kutoa.
Uwezo wa kamera wa simu hii ni mzuri sana ukilinganisha na simu zao za nyuma. Kwa fununu zilizopo ni kwamba kamera yake ya selfie (mbele) itakuwa na MP 16 wakati kamera yake ya nyuma itakuwa na MP 23.
Ukiachana na fununu hizi kampuni ilituma picha katika mtandao wa Twitter ambayo ilipigwa na simu hii.
Jionee Picha Hiyo.
Can you tell which photo was taken with the OnePlus 5? pic.twitter.com/Pd27la4ewn
— OnePlus (@oneplus) May 29, 2017
Japokuwa hawakuweka wazi juu ya picha hizo kwamba ni ipi ambayo imepigwa na OnePlus 5, hili limebaki kama swali kwa watumiaji.