Open YOLO: Google inataka kukusaidia Kusimamia Password zako

0
Sambaza

Kusahau password ni jambo linalowakuta wengi? Google inataka kukusaidia kutokumbuka password zako. Fahamu kuhusu Open YOLO!

Soma pia –

1. Jinsi Ya Kutengeneza Neno Siri (Password) Imara!

2. Makosa katika utengenezaji wa password za Simu na

Open YOLO

Muungano wa Dashlane na Google katika ujio wa teknolojia itakayoondoa ulazima wa utumiaji wa passwords nyingi katika apps ndani ya Android

Google wanaungana na kampuni inayomiliki app ya kusimamia nywila (Password manager) ifahamikayo kama Dashlane kuhakikisha watumiaji wa Android hawatakuwa na ulazima wa kukumbuka password zao katika kutumia (log in) katika apps mbalimbali.

Wamekuja na kitu kinaitwa Open Yolo – yaani ‘You Only Log In‘…wakimaanisha uta’login mara moja tuu katika simu yako na kisha katika apps zote unazotumia hautaulizwa tena masuala ya password.

SOMA PIA:  Jinsi Ya Ku'Log Out' Instagram Kwa Kutumia Kifaa Kingine!

Mpango (project) huo unahusisha makampuni mbalimbali yanayotoa huduma/apps zinazowasaidia watu kutengeneza na kuhifadhi passwords wanazotumia katika mitandao mbalimbali.

Apps/huduma za kuhifadhi na kusimamia passwords (password managers) kama vile Dashlane, LastPass na 1Password, zote zinakusaidia kusimamia masuala ya passwords zako na kupitia mpango wa Open Yolo basi haitajalisha huduma unayotumia hautalazimika kuingiza password.

Ingawa nia ya jambo hili ni zuri ila bado linaleta wasiwasi kiusalama kama mdukuzi akifanikiwa kuingia kwa kutumia mfumo huu..kwani huduma nyingi zinaweza athirika kwa wakati mmoja. Ila tuna uhakika Google tayari ashaliona hili na watakuwa wamejipanga vizuri kiusalama.

SOMA PIA:  Google yafanya mabadiliko muonekano wa tovuti yake katika simu janja

Soma pia –

1. Jinsi Ya Kutengeneza Neno Siri (Password) Imara!

2. Makosa katika utengenezaji wa password za Simu na

Endelea kutembelea TeknoKona kwa habari na maujanja kila siku. Tufuatilie pia kupitia Twitter, Instagram na Facebook. Kumbuka ku’share na wengine

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com