OPPO F3 FCB: Simu maalum kwa mashabiki wa FC Barcelona

0
Sambaza

Kampuni ya uzalishaji wa simu za OPPO imetoa simu maalumu kwa ajili ya kuadhimisha mafanikio ya klabu maarufu duniani ya soka ya FC Barcelona inayoitwa OPPO F3 Barcelona.

OPPO ni mmoja wa washirika wa kibiashara wa timu ya FC Barcelona au Barca ya nchini Uhispania inayoshiriki ligi kuu maarufu duniani ya La Liga.

Afisa Mkuu Mtendaji wa OPPO nchini Srilanka Tom Zou alisema, “Tunajivunia kuwa mmoja wa washirika wa FC Barcelona timu inayoungwa mkono na watu wengi duniani.”

SOMA PIA:  Alama za vidole kimeo katika simu za Pixel 2 baada ya kusasisha Android 8.1

Aidha aliongeza kusema, “simu hii si tu kwa washabiki wa klabu ya FC Barcelona tu bali kwa watu wote wenye kuupenda mchezo wa mpira wa miguu kote duniani”.

OPPO F3 Barcelona imezinduliwa mwaka huu katika sehemu mbalimbali Duniani na imeanza kuuzwa katika masoko kadhaa.

Simu hiyo ambayo haitakuwa na muendelezo (Toleo maalum tu) imenakshiwa kwa rangi nyekundu na dhahabu ambazo ni moja ya rangi za Klabu hiyo.

Sifa za simu hiyo ni kama ifuatavyo

  • Kamera ya mbele– Zipo mbili moja ya 16MP na 8 MP
  • Kamera ya nyuma– 13MP
  • Ukubwa wa uhifadhi wa ndani– 64GB
  • Unaweza kuongeza ujazo– Mpaka wa 128GB
  • Mfumo Endeshi– ColorOS 3.0 based on Android 6.0 Marshmallow
  • Ukubwa wa RAM– 4GB
  • Prosesa– 1.5GHz Octa-Core (MTK)
  • Ukubwa wa kioo– Inchi 5.5
  • Uwezo wa Betri- Li-ion 3200mAh
  • Mfumo wa Ulinzi– Fingerprint Scanner
SOMA PIA:  Jinsi Ya Ku'Block Simu Katika iOs Bila Ya Kutumia App! #iPhone

Simu Janja hii tayari kwa soko la Afrika Mashariki imeshazinduliwa na kuanza kuuzwa. Kwa sasa inapatikana katika masoko ya nchi ya Kenya kwa pesa ya huko kwa Shilingi 39,999.

Kazi kwenu washabiki wa FC Barcelona kuhakikisha mnaipata simu Janja hiyo kuonesha ushabiki wa damu wa timu hiyo nguli na maarufu kwa staili za pasi za Tiki-Taka.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com