Baada ya uzinduzi wa Vivo V9 na Samsung Galaxy J7 prime 2 nchini India, Oppo nayo imekuchukua nafasi ya kuonesha upinzani wake kwa wengine.
Oppo imezindua simu janja yake inayotambulika kama Oppo F7. Simu hii bila shaka itawavutia wale wenye kupenda kujipiga Selfie kwani ina MegaPixel za kutosha. Kamera ya mbele (Selfie) ina MegaPixel 25 hivyo kuifanya picha itakayopigwa kuweza kukuzwa zaidi na bado ubora wake hautapotea.
Kamera yake ya nyuma pia ipo vizuri kwani ina MegaPixel 16. Kwa upande wa kioo kina ukubwa wa inchi 6.2 na ni Full HD+ (1080×2280 pixels).
Prosesa yake itakuwa ni 2GHz MediaTek Helio P60 octa-core na mfumo endeshi utakuwa ni wa Android toleo la Oreo.
Sifa nyinginezo za simu hii ni kuwa na Betri ya ujazo wa 3,400mAh, Wi-Fi, Bluetooth, 4G VoLTE pamoja ulinzi wa mguso wa vidole (Fingerprint).
Ukubwa wa kioo: 6.2-inch
Prosesa: MediaTek Helio P60 octa-core
Ujazo wa Ram: 4GB/6GB RAM
Ujazo wa uhifadhi: 64GB/128GB
Kamera ya nyuma: 16MP
Kamera ya mbele: 25MP
Ujazo wa Betri: 3400mAh
Bei yake na muda wa kuuzwa
Oppo F7 itakuwa inapatikana kwenye maduka ya mtandaoni na nje ya mtandao yaani maduka ya kawaida kuanzia Aprili 9 mwaka huu.