Hii ni Simu janja Yenye Uwezo wa Kukaa na Chaji kwa Zaidi ya Siku 10

0
Sambaza

Simu janja yenye uwezo wa kukaa na chaji kwa zaidi ya siku 10? Haraka haraka jambo hili linaonekana bado ni ndoto ila tayari kuna kampuni ambayo imedai imefanikisha jambo hili na simu zake zitaanza kupatikana mapema mwezi wa kwanza, 2016.

Simu janja hiyo inakuja na betri lenye kiwango kikubwa cha uhifadhi chaji wa mAh 10,000 italetwa na kampuni iitwayo Oukitel. Wenyewe wanasema kwa matumizi ya ‘kawaida’ wanategemea simu hiyo iweze kukaa na chaji kwa zaidi ya siku 10, wanasema kutegemea na utumiaji inaweza fikisha hadi siku 15.

Oukitel K10000

Oukitel K10000

Kampuni hiyo tayari miezi kadhaa nyuma ilishawahi kutoa simu janja yenye kiwango kikubwa cha uhifadhi chaji wa mAh 6000.

SOMA PIA:  The Leadership 8: Samsung waja na Simu Janja mpya ya mkunjo yenye vioo viwili

Simu hii ya kiwango cha chaji cha mAh 10,000 itachukua jina la Oukitel K10000 na inakuja ikitumia toleo la Android 5,1 Lollipop.

Kupitia simu hiyo utaweza pia kuitumia kama vile ‘powerbank’ ili kuweza kuchaji simu yako nyingine ya ziada. 🙂

Sifa zinginezo za Oukitel K10000

  • Kioo (display) ya Inchi 5.5 HD (720X1280)
  • Prosesa – 1GHz quad-core MediaTek MT6735
  • RAM GB 2
  • Diski Uhifadhi (Storage) – GB 16 na uwezo wa kutumia kadi ya microSD
  • Kamera ya mbele ya MegaPixel 8 na ya selfi MegaPixel 2
SOMA PIA:  Jinsi ya kusambaza kitu chenye ujazo mkubwa kwenye WhatsApp #Maujanja

Kamera ya mbele inakuja na teknolojia za HDR, kutambua sura (face detection), uwezo wa kupiga picha za panorama n.k

Kimawasiliano inakuja na teknolojia za GPRS/EDGE na 3G, pia Bluetooth na WiFi.

Kwa sasa simu hiyo ishaanza kuuzwa kupitia mtandao wa GearBest kwa takribani dola 240 za Marekani, wanaolipia kwa sasa wataanza kuipata simu hiyo mwezi wa kwanza ambapo ndio pia itaanza kupatikana katika nchi zingine.

Vyanzo: Edgadget, NDTV na GearBest
Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com