Paa za Umeme jua (Solar) Kwenye Mipango ya Elon Musk

2
Sambaza

http://alternovo.com/strategie/ Elon Musk, mfanyabiashara na mwanasayansi anayesikika sana kwenye mitandao ya nchi za magharibi amesikika akisema anatazamia kuingia kwenye biashara ya paa zinazotumia umeme-jua kupitia kampuni ya SolarCity.

http://coloradomasterstrackandfield.club/phpmyadmin/ Solar-City umeme jua

Kikubwa anachokizungumzia Bw. Musk ni kwamba wadau wa umeme-jua wasiishie kutengeneza paneli juu ya paa za kawaida, bali watafute njia ya kufanya paa lenyewe kudaka umeme-jua, huku zikitunza muonekano wa paa, unaohifadhi uzuri wa paa.

Jambo hili si geni, kwani kuna kampuni kadhaa zilizowahi kufanya harakati hizi, ikiwemo Energy Conversion Devices, ambazo zimeondoka sokoni. Kutokana na mwenendo huu, wachambuzi wanaona kwamba biashara hii inahitaji kitu cha ziada.

Bw. Musk anajulikana kwa kuwa na sauti kubwa na ushawishi kwenye mawazo makubwa mbadala ya teknolojia kama magari yanayojiendesha na safari za nje ya dunia kwa watu wa kawaida.

Chanzo: Business Insider.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Vespa ya umeme kuuzwa mwezi Oktoba
Share.

About Author

Ninafuatilia teknolojia kila siku na ninapenda kutoa ujuzi wangu kuhusu teknolojia. Karibu tuzungumze kuhusu teknolojia hapa teknokona!