fbpx

Panasonic yazindua tabiti mbili kwa mara moja

0

Sambaza

Panasonic ni moja ya makampuni ambayo bidhaa zake hasa za kiganjani hazijaenea katika nchi za Afrika kulinganisha na washindani wengine na hivi karibuni imezindua tabiti mbili kwa mkupuo.

Tabiti ambazo zimezoeleka na hata kupatikana kwa wingi ni za Huawei, Tecno, Samsung, Vodafone, n.k lakini ni nadra sana kumkuta mtu akimiliki tabiti ya Panasonic lakini mambo huwenda yakawa ni tofauti katika siku za usoni.

Tabiti hizo mbili zilizozinduliwa kwa mkupuo ni Panasonic T1 na L1 ambazo zote zimeelezwa kuwa na uwezo wa kubadilisha betri ya kuhitaji kuzima na kuwasha.

tabiti mbili

Tabiti mbili za Pnasonic; T1 na L1.

Sifa za tabiti T1 na L1 kutoka Panasonic.

Tofauti ya tabiti hizi mbili (T1 na L1) ni ndogo sana lakini ambayo ni rahisi zaidi kuiona ni urefu wa kila tabiti; T1 ina urefu wa inchi 5 na L1 ina inchi 7, tofauti na hapo zina sifa sawa kila kipengele.

tabiti mbili

Tabiti ya Panasonic T1 yenye urefu wa inchi 5 pia ina uwezo wa kutoingia vumbi/maji kwa kina fulani.

  • Recommended Site Prosesa: Qualcomm Snapdragon CPU ARM Cortez-A7 Quad-Core 1.1 GHz
  • http://rossgraphicdesigner.com/rgd-logok-3/ Programu Endeshi: Android 8.1 Oreo
  • RAM: GB 2
  • Memori ya ndani: GB 16 (uhifadhi wa ziada wa mpka GB 64)
  • Uwezo wa betri: 3,200mAh
  • Teknolojia nyinginezo: GPS, Bluetooth 4.2, inatumia kadi ndogo ya simu, NFC

    tabiti mbili

    Tabiti ya Panasonic L1 yenye urefu wa inchi 7 pia ina uwezo wa kutoingia vumbi/maji kwa kina fulani.

Tabiti zote mbili hazijafahamika ni lini zitaanza kuuzwa lakini inategemea kuingia sokoni miezi michache ijayo na bei zake zintazamiwa kuwa zaidi ya $1,400|Tsh. 3,220,000.

Vyanzo: ZDNet, Engadget

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Meizu Zero: Simu isiyokuwa na mengi tuliyoyazoea
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.