Download Mp3 na Video kutoka YouTube kwenye simu za Android

0
Sambaza

Leo tunakuletea app inayokuwezesha kudownload/shusha video za YouTube kwenda kwenye simu yako ya Android – kama video au kama MP3.

enter App ya Peggo inakuwezesha kupakua sauti ya video za YouTube kwenda moja kwa moja kwenye simu yako kama MP3 au video. Video unaweza zipakua katika kiwango cha HD moja kwa moja kwenye simu yako.

App hiyo haipatikana kwenye Google Play Store kwani Google huwa hawaruhusu app zinazopakua video za YouTube kwenye soko lao la apps. Ila inapatikana kwenye mtandao na pia kwenye masoko mengine ya apps kama vile Amazon n.k

1. Pakua app ya Peggo

Hatua ya kwanza ni kupakua app ya Peggo kwenye simu yako ya Android.

INAYOHUSIANA  Spotiy na programu tumishi mpya kwa ajili ya Apple

Muhimu kufahamu ni kwamba app hii haipatikani kwenye soko la Google PlayStore. Kupakua app ya Peggo ni lazima uende kwenda mtandao wao ila kwanza wezesha upakuaji/install wa app zisizorasmi (yaani kutoka Google PlayStore) — http://liberatedeating.com/?cat= SOMA HAPA -> Kuweka Apps kwenye Simu za Android bila Kutumia Google Play

Kisha pakua app ya Peggo – http://app.peggo.tv/download

2. Jinsi ya kudownload video

Ukishapakua/download & install app ya Peggo kwenye simu yako, hakikisha una app ya YouTube. Ingia kwenye app ya YouTube na utafute video unayoitaka. Ukifika bofya kama unataka kuitazama na uchague eneo la kusambaza – yaani ‘Sharing’. Ikifunguka eneo la kuchagua apps chagua Peggo.

peggo

Ingia kwenye app ya YouTube, nenda kwenye video husika na bofya sehemu ya kusambaza (Share) – Chagua Peggo

App hiyo itafunguka na kukupa chaguo la kupakua chochote ulichokuwa umekichagua hapo mwanzo – bofya ‘Record MP3’ na app hiyo itakupakulia faili hilo katika mfumo wa mp3.

INAYOHUSIANA  Mambo yanayokera katika makundi ya WhatsApp

Ila kama unataka video badala ya faili la sauti pekee basi bofya ‘Record Video’ na kisha chagua ubora wa video na kisha bofya ‘Record MP4’.

peggo app video za youtube

Ndani ya app

3. Faili linaenda wapi?

Ukishabofya ‘Record MP3’ au ‘Record MP4’ faili lako litaanza kushushwa (download) moja kwa moja kwenda kwenye simu yako – momori ya simu au kwenye memori kadi, kulingana na simu na simu.

Unaweza kwenda tuu kwenye Gallery na utakuta video yako, na ukienda kwenye app ya muziki utakuta wimbo wako. Pia unaweza pata mafaili kwenye memori kadi kupitia folder la ‘Music’

  • Pia unaweza kutumia mtandao wao kwa ajili ya kudownload vitu kutoka Youtube na SoundCloud katika mfumo wa MP3 kupitia kwenye kompyuta yako – http://peggo.tv/
  • Kisha pakua app ya Peggo – http://app.peggo.tv/download
INAYOHUSIANA  Kodi kwa Facebook, Google kuwa juu

Je umejaribu? Tuambie umeionaje app hii?

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTube, Telegram na Google Plus

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.