Pengine Google Inaweza Ikainunua Kampuni Ya HTC!

0
Sambaza

Biashara ya kutengeneza na kuuza simu ina changamoto nyingi sana. Fikiria hapo awali majina makubwa kama vile Nokia na BlackBerry yalivyokuwa yametawala lakini sasa kila mmoja anafanya mpango wa kujirudisha katika mchezo.

Inavyoonekana katika biashara hii ukishindwa kuwa mbunifu na kuleta kitu kipya sokoni basi unaweza ukasahaulika ndani ya muda mchache sana.

Google

Pengine kampuni ya HTC imeliona hilo kwani labda wameona dhahiri kuwa kwa sasa hawawezi kushindana moja kwa moja na kampuni kubwa kama vile Apple na Samsung. Inaweza ikachukua muda tuu na kampuni ikajikuta ipo katika sehemu sawa na Nokia au hata Blackberry.

SOMA PIA:  YouTube GO - App ya YouTube isiyokula data sana

Pengine hali hii ya uoga ndio itakayoipelekea kampuni kufanya maamuzi haraka, na je maamuzi hayo ni yapi?

Google ina sababu nyingi tuu za kulinunua kampuni hilo. Kwanza kabisa inabidi tujue kuwa Google na wao wanatengeneza simu janja zao zinazofahamika kama Pixel. Kwa kutumia HTC inaweza ikaboresha simu hizo karibia kila kitu (Hardware, Software, Network, Cloud .n.k)

Vile vile kumbuka HTC hawana simu janja tuu vile vile wana teknolojia ya VR (Virtual Reality) ambayo pia inasemekana inawezekana ikanunuliwa na Google.

SOMA PIA:  Google waliuza simu za Pixel takribani milioni 4 mwaka 2017

Vyanzo vinasema kuwa Google inaweza ikanunua teknolojia hiyo tuu na kuachana na simu za HTC. Hii pia imewashangaza watu kwani Google bado wana teknolojia ya VR. lakini kama hili likitokea itakua sio mbaya kwani itazidi kuongeza ushindani kwa wapinzani.

Ningependa kusikia kutoka kwako, kama ingebidi kimoja kinunuliwe wewe unaona ni kipi sahihi zaidi (Simu, VR)? niandikie hapo chini sehemu ya comment.

Tembelea TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com