Phab2 Pro: Google na Lenovo waja na Augmented Reality ktk Simu

Phab2 Pro: Google na Lenovo wazindua simu janja yenye teknolojia ya ‘Augmented reality’

0
Sambaza

Simu janja zinazidi kubeba teknolojia za kisasa sana na Google na Lenovo wanazidi kutuonesha ni jinsi gani teknolojia kubwa na za kisasa zinaweza ingizwa kwenye simu janja mapema sana.

Lenovo simu Phab2

buy herbal Seroquel Muonekano wa nyuma wa simu hiyo ya Phab2

Je ushasikia kuhusu teknolojia ya Virtual Reality (VR) inayohusisha uvaaji wa kitu na kuweza kuona mambo kama vile na wewe upo katika eneo hilo? Augmented Reality (AR) ni teknolojia inayowezesha hilo bila uvaaji wa kitu.

http://dorothy6.com/event/every-wednesday-is-ladies-night/ Teknolojia ya Augmented Reality (AR) kwa ajili ya kwenye simu imekuwa ikitengenezwa na Google na mpango (project) huo wameipa jina la Tango Project.

phab2 pro

go site Watafiti kutoka Lenovo wakifanya presentation

Simu ya Phab2 Pro kutoka Lenovo imekuwa ndio simu ya kwanza kuingia sokoni ikiwa na teknolojia ya Tango project ndani yake.

Simu hiyo ya inchi 6.4 tayari inakuja na apps 25 zenye uwezo wa kutumia uwezo wa teknolojia hiyo ya AR na wenyewe Lenovo wanasema lengo ni kufikia apps 100 kufikia mwisho wa mwaka huu.

phab 2 pro

Mchanganyiko wa vitu halisi na vya ‘virtual….katika Phab 2

Mkurugenzi kutoka kitengo cha engineering anayefanya kazi Google Bw. John Lee amesema kuwa teknolojia ya Tango itawezesha simu janja walizozitengeneza kuweza kutambua mahali zilipo na hivyo basi kuweza kubadilisha mazoea ya mtumiaji jinsi ambavyo huwa anakabiliana (interact) na vile vinavyomzunguka mbele yake.

Simu hiyo inatumia teknolojia za ‘depth sensor’ na ‘motion sensor’ kuiwezesha kamera yake kutambua eneo ulilopo katika chumba na kisha kukuonesha ‘virtual objects’ kutumia teknolojia hiyo ya Augmented Reality

INAYOHUSIANA  WhatsApp: Kupiga simu kwa njia ya sauti/video kwenye makundi inawezekana

Phab2 Pro itaanza kupatikana sokoni kuanzia mwezi wa tisa mwaka huu. Bei ni dola 499 za Kimarekani (takribani Tsh 1,100,000/= | Ksh 50,400/=)

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.