Piga Selfie Na Itumie Kama Emoji Na App Ya Allo!

0
Sambaza

Najua kwa dunia ya sasa Emoji ndio kila kitu katika kutuma na kupokea mesiji tukiwa katika mitaandao. Ukiwa na kifaa chenye Emoji nzuri zaidi na za kijanja pia inakufanya ujisikie vizuri sio?

Ukiachana na BitEmoj kuna  wale ambao wanapenda kwa namna moja au nyingine emoji za vifaa vyao ziwe na chembechembe ya ufanano na sure zao halisi. Njia ni rahisi kabisa na TeknoKona inakuletea maujuzi hayo.

Google wametambulisha kipengele kipya katika App yao inayojulikana kama Allo Messeging App. Sawa najua kwa kina kabisa pengine labda hutumii App hii ya Allo lakini kitu kizuri ni kwamba unaweza ukaburudika kutumia App hii kwa kiasi kikubwa sana

SOMA PIA:  Cubimorph: Fikiria kuwa na simu yenye uwezo wa kukunjwa na kupangwa vile upendavyo

Cha Kwanza kabisa cha kufunya ni kwenda katika soko la Google Play Store na kisha shusha App hii

Ukishafanikiwa fungua App na fanya kama unamtumia mtu meseji. Chagua katika kilama cha Emoticon  baada ta hapo ingia katika kialama cha emoji ambacho pembeni yake kuna kialama cha kamera na kisha utapelekwa katika uwanja mpya.

Bonyeza katika eneo la Create na kisha kamera yako itafunguka. utayaona maduara mawili ambayo utalengesha uso wako ili macho yaendane sambamba na hayo maduara na kisha piga picha.

SOMA PIA:  Google AutoDraw: Sasa hivi mtu yeyote anaweza kuwa mchoraji mzuri

picha itapigwa na emoji zitajitengeneza ila kama hukuzipenda unaweza ukabonyeza Customize ili kuziongezea au kuzipunguzia vitu ili kuendana na wewe jinsi ulivyo mfano shepu ya sura yako, rangi ya nywele nk. Ukimaliza zoezi hilo bonyeza Save.

Ukimaliza App itakurudisha katika uwanja wako wa meseji na hapo ndipo unapoweza kutumia hizo emoji zenye sura yako wakati una tuma meseji zako.

Kama mtu mwingine hatumii emoji za Allo ukimtumia meseji tuu yenye emoji basi sambammba itamfikia na link ambayo akiifuata itamsaidia kuweza kushusha App hiyo nae aweze kupata uhondo huo.

SOMA PIA:  Tahadhari: Password meters si za kuaminika kwa asilimia zote

Allo Google Play Store

iOS – Lakini usishangae kama kipengele hiki bado, kipo njiani

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini sehemu ya comment, ungejisikiaje pale unapoweza kutumia Emoji zenye sura yako kabisa wakati wa kutuma meseji?

Tembelea TeknoKona kila siku kwani daima tupo nawe katika teknolojia!.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com