Pixel 2: Google watambulisha moja ya simu bora zaidi kwa mwaka 2017

Pixel 2: Google watambulisha moja ya simu bora zaidi kwa mwaka 2017

0
Sambaza

Amini usiamini, simu mpya kutoka Google za Google Pixel 2 na Pixel 2 XL zinashindana na ata kuzipita simu za iPhone X, LG V30 na ata Samsung Galaxy Note 8.

http://ohiopawnshops.net/2015/12/ Baada ya mafanikio ya kipekee ya uletaji bidhaa kwa Google baada ya kuleta simu ya Google Pixel 1, utengenezaji na utambulisho wa toleo la pili la simu ya familia ya Pixel ilikuwa imeshalenga kuwa ya kitofauti na kuweza kushindana na simu ambazo zimeshatangazwa na Apple – iPhone X na ata na Samsung – Note 8.

simu google pixel 2

Muonekano wa nyuma wa simu ya Google Pixel 2

Sifa zake;

Programu endeshaji

Simu zote zinakuja na toleo jipya kabisa la Android 8.0.

Kamera

Moja ya sehemu kubwa sana na ya juu kuzidi simu zingine zilizopo sokoni kwa sasa. Kwenye Pixel 2 na Pixel 2 XL Google wamehakikisha simu hizi zina kamera yenye ubora wa juu zaidi kuzidi simu zingine nyingi zilizopo sokoni kwa sasa.

INAYOHUSIANA  Clickfarms: Wauza Likes, Shares, na Comments wakamatwa nchini Thailand

Huduma mbalimbali za kupima ubora wa kamera za simu zimeweka wazi data zinazoonesha Google Pixel 2 kuwa na kamera bora zaidi kuzidi Galaxy Note 8 na ata simu mpya kabisa ya hadhi ya juu kutoka Apple ya iPhone X. (mfano DXOMARK)

picha simu pixel 2

Kamera yake ina kiwango na ubora wa juu wa kuweka rangi sahihi ata kama picha imepigwa muda ambao simu haijatulia sana (stablization) na ata kama imepigwa kwenye mazingira yenye mwanga na giza pia.

Ukubwa

Simu za Google Pixel 2 na Pixel 2 XL hazina tofauti sana, tofauti kubwa kati yake ni ukubwa wa simu husika. XL ni kubwa zaidi. Ila mambo mengi ya ndani ya simu ni kiwango kimoja. Kwenye betri na ukubwa wa simu ndio kuna tofauti sana.

simu google pixel 2

Muonekano simu ya Google Pixel 2

Pixel 2 ina ukubwa wa inchi 5 (pixels 1,920 kwa pixels 1080) wakati Pixel 2 XL ina ukubwa wa inchi 6 (pixels 2,880 kwa pixels 1,440), sifa zingine angalia hapa chini.

Google Pixel 2 vs Pixel 2 XL

Google Pixel 2 vs Pixel 2 XL

Rangi kuna: Nyeusi, Nyeupe na ya blu.

google pixel 2

Muonekano wa simu za Google Pixel, rangi tatu.

Diski uhifadhi

Simu hizi sinapatikana kwa ukubwa wa aina mbili, GB 64 na GB 128. Pixel 2 ya GB 64 ni dola 649 za Marekani (Takribani Tsh 1,500,000) na ya ukubwa wa GB 128 ni dola 749 (takribani Tsh 1,700,000).

where can i purchase doxycycline hyclate Kwa Pixel 2 XL ni dola 849 kwa toleo la GB 64 (takribani Tsh 1,900,000/=) wakati toleo la GB 128 ni dola 949 (takribani Tsh 2,150,000/=)

Hakuna tena eneo la kuchomoka spika za masikio (earphones).

INAYOHUSIANA  Panasonic yazindua tabiti mbili kwa mara moja

Ni badiliko ambalo lilianzia kwa Apple na wengi waliliponda, ila sasa na Google pia wamelichukua. Simu za Pixels 2 hazina sehemu ya kuchomeka earphones, sababu kuu ni kuwezesha simu hizi kuwa nyembamba zaidi na kupata nafasi ya kuweka betri kubwa zaidi.

http://grownupinsights.com/2016/03/how-do-you-plan-on-accomplishing-your-goals/ Ila pia kama uwezi kutumia earphones kwa njia za Bluetooth basi utaweza kutumia kawaya spesheli kupitia adapter inayopita sehemu ya kuchajia simu hizi.

Ujazo wa bure kupitia Google Photos (Drive) wa picha zako

Ukiwa na simu hizi usihofu suala la ujazo wa simu. Utaweza kuhifadhi nakala za picha na video zako kupitia huduma ya Google Photos ata kwa picha na video za ubora wa juu bure kabisa – bila kizuizi, MILELE!

INAYOHUSIANA  Smile Telecom ya Uganda yawalipia wateja wake kodi ya mitandao kwa miezi mitatu

Hii ni ofa tamu kabisa kwa wapenda kupiga picha sana, Apple kupitia iPhone wanatoa huduma kama hii ila yao mwisho ni GB 5 tuu.

Je wewe umezipokeaje simu hizi? Tunazidi kuona simu janja za viwango vya juu zinatoka ila changamoto kubwa ni bei zake. Je wewe unalionaje suala hili pia?

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.