Pixel Buds; Spika za masikioni zenye uwezo wa kutafsiri lugha

1
Sambaza

Lugha ni moja ya kikwazo kikubwa katika mawasiliano kwani kwa dunia ya leo inampasa mtu aweze kujua lugha zaidi ya moja (hasa zile zenye zinazojulikana na wengi) ili kuweza kujichanganya sehemu mbalimbali/kuaminika, kupata ujuzi, n.k.

Ukuaji wa teknolojia umefanya kwa kiasi fulani umefanya umuhimu wa Mkalimani kufifia kutokana na kwamba hivi sasa inawezekana kupata tafrsiri ya neno/sentesi kutoka lugha moja hadi nyingine kwa urahisi zaidi bila kusumbuka ilimradi tu uwe na intaneti au hata bila ya intaneti unaweza ukapata tafsiri kupitia programu tumishi mahususi kwa ajili ya tafsiri.

SOMA PIA:  Gari la Mitsubishi Outlander linaweza kudukuliwa kwa njia ya WiFi

Pixel Buds zimetengenezwa na nani? (Sifa za Pixel Buds)

Mwezi Oktoba umekuwa ni ‘Mvua’ ya uzinduzi wa bidhaa mbalimbali kwa upande wa Google ambao ndio wametengenezea spika za masikioni zenye uwezo wa kipekee kabisa wa kutafsiri lugha.

Zinafanya kazi kwenye simu janja yoyote kwa njia ya bluetooth na zinaweza kutumika kusikilizia muziki, kuongelea kwenye simu, kutumika kwenye kisaidizi binafsi cha Google na kubwa zaidi kuweza kuelewa lugha mbalimbali (kutafsiri).

Zilizinduliwa kwa pamoja na simu janja mbili kutoka Google, kompyuta ya mpakato ambayo inaweza kufanya kazi sawa na ile programu ijulikanayo kama SIRI. Bidhaa zote hizi 3 zimetengenezwa na Google.

Kwa kutumia programu mpya, Google Assistant zinaweza kutafsiri chochote kutoka kwenye programu hiyo kwa lugha mbalimbali.

Jinsi Pixel Buds zinavyofanya kazi.

Haihitaji nguvu wala akili nyingi kuweza kujua jinsi gani spika za masikioni kutoka Google zinavyofanya kazi ile iliyokusudiwa. Kwa kubonyeza kitufe kilichopo kwenye moja ya spika hizo na huku ukiwa umeiunganisha na Google assistant/Google Translate na kisha kusema mathalani “Let me speak Italian”, hapo mtumiaji ataongea kwa Kiingereza na kusikia tafsiri yake kwa Kitaliano.

SOMA PIA:  Backup and Sync: App/Programu Mpya ya Google Drive yaja

Unaweza pia ukauliza swali huku ukiwa umeunganisha spika hizo na Google Assistant bila kusahau kushikilia kile kitufe cha kwenye moja ya spika na hapo utaweza kupata jibu/majibu ya swali lako.

Pixel Buds ni spika za masikioni ambazo kwanza ni wireless (zinaunganishwa kwa njia ya Bluetooth) lakini pia kupitia app ya Google kwa ajili ya kutafsiri (Google Translate) ina uwezo wa kutafsiri lugha takribani arobaini (40).

Bonyeza kitufe na kisha sikiliza ili kuweza kupata huduma ya tafsiri au majibu ya kile ulichouliza.

Umezipenda? Basi huna budi kuvuta subira mpaka Novemba 22 zitakapoanza kuuzwa na gharama yake ni $159|Tsh. 357,591. Je, unadhani spika hizi za masikioni zitakuwa gumzo ulimwenguni kutokana na kuwa na uwezo wa kutafsiri lugha?

Vyanzo: The Verge, Telegraph

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com