Pixelbook: Kompyuta ya kwanza kutoka Google yenye 'Kisaidizi binafsi'

Pixelbook: Kompyuta ya kwanza kutoka Google yenye ‘Kisaidizi binafsi’

3
Sambaza

Ushindani ndio siku zote unamfanya mtu/kampuni awe bora zaidi na kuendelea kuleta ushindani au hata kumzidi mwenzake ambaye wanafanya kitu/biashara inayofanana. Google ndivyo alivyoamua kuweka kwa mara ya kwanza “Google Assistant”.

Pixelbook ni kompyuta mpakato yenye vitu vingi vya kuvutia lakini kubwa zaidi ni kuhusu Google kuamua kwa mara ya kwanza tena follow kompyuta hiyo ina kalamu maalum kwa ajili ya kuweza kutumia kwenye kioo badala ya kutumia vidole.

Mwaka 2013 ndio Google ilianza kutoa kompyuta zake mbazo zinatumia programu endeshi (ChromeOS) yake mwenyewe na tangu hapo imekuwa ikifanya hivyo mpaka hivi leo.

Pixelbook inamuwezesha kutumia apps kama Instagram, Snapchat kupitia kwenye kompyuta (Unaweza ukapakua apps hizo kupitia kwenye Play Store kama ilivyo kwenye simu janja).

 Yaliyomo kwenye kompyuta pakato Pixelbook.

1. best place to buy dapoxetine Google Assistant. Hii ni programu tumishi ambayo inakuwezesha kutafuta kitu chochote kwenye kompyuta (Piexelbook) baada ya kutamka “OK, Google” na kisha kuanza kutoa maelekezo unataka ikutafutie nini kwenye kompyuta/kitu chochote kutoka mtandaoni. Pia unaweza ukatumia go to link funguo maalum ya kisaidizi hicho kitakachokuwezesha kuandika kile unachojaribu kukitafuta kwenye kompyuta.

INAYOHUSIANA  WhatsApp: Kupiga simu kwa njia ya sauti/video kwenye makundi inawezekana

Google Assistant inafanya kazi na ile programu tumishi inayopatikana kwenye vifaa vya Apple (SIRI). Vilevile Google assistant itaanza kupatikana kwenye kompyuta za Chromebook kuanzia mwaka 2018.

2. Pixelbook Pen. Kalamu mahususi inakayokuwezesha kuchora, kuandika kushusha/kupandisha ukurasa. Microsoft Surace na iPad Pro pia vina kalamu maalum kwa ajili ya kumfanya mtumiaji afurahie kifaa hicho.

Baadhi tu ya vitu unavyoweza kufanya kwa kutumia Pixelbook Pen kwenye kompyuta mpya kutoka Google.

3. Prosesa. Kivutio cha wengi hasa wanaojua vizuri kompyuta nzuri inatakiwa iwe na vigezo gani basi moja ya vitu amabvyo watakuwa wanashauku ya kutaka kujua ni upande wa prosesa, kwamba kopyuta hiyo ina prosesa ya mfumo gani? Pixelbook inaanzia core i5 na core i7 kutoka Intel pamoja na RAM ni GB 8.

INAYOHUSIANA  Biashara ya kwanza kufanyika mtandaoni

4. Programu tumishi kutoka Google Playstore. Google waamua kuongeza programu tumishi kwenye soko la programu tumishi ambazo unaweza kutumia kwenye Pixelbook bila kusahau apps maarufu kama vile Instagram na Snapchat.

Tweet kutoka akaunti rasmi ya Google ikizungumzia kompyuta mpakato iliyozinduliwa hivi karibuni huko San Francisco, Marekani.

Sifa nyinginezo za Pixelbook ni kwamba betri yake inadumu kwa saa 10 na chaji vilevile Pixelbook Pen inauzwa bei tofauti na kompyuta yenyewe, ni $131 sawa na Tsh. 294,619.

Kwa ujumla ni kompyuta yenye uwezo mkuwa na kwa hakika italeta ushindani. Bei yake ni kuanzia $1,315 (Intel core i5 yenye 128 GB SSD), $1,579 (Intel core i5 yenye 256GB SSD) mpaka $2,237 (Intel core i7 yenye 512GB HDD).

Vyanzo: Telegraph, The Verge

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|