Post Picha Moja Instagram Ikiwa Imegawanyika Katika Vipande Tisa (9)! #Android #iOs

0
Sambaza

Instagram bado inasimama kama mtandao namba moja duniani kwa maswala ya picha na video. Kwa umaarufu huo, umegeuka kuwa kimbilio la watu wengi wanaopenda mitandao ya kijamii.

Kuna aina tofauti tofauti watu wanaweza kuzitumia katika ku’post matukio yao. Kubwa ambali limenifurahisha ni kwamba kwa msaada wa App au ujuzi wa mtu binafsi unaweza ukapost picha moja ila ikajigawa mara 9 na kila kipande kikajipost ili kutengeneza picha moja

Pengine labda hujanielewa! Tazama picha hapo chini kupata picha zaidi!

Baada ya kupata pich atwende moja kwa moja katika App ambazo utaweza kuzitumia katika kuwezesha hili.

SOMA PIA:  Jiandae kwa Matangazo ndani ya Facebook Messenger

Kwa Wale Wa Android.

  1. Instagrid Grids For Instagram

Instagrid Kwa Android

Hii ni moja kati ya App maarufu sana ambayo inapatikana bure. Ikiwa imeshushwa zaidi ya mara milioni moja itakusaidia kutengeneza picha hizo bila ya kupoteza ubora wa picha zenyewe. Kingine kikubwa ni kwamba hutatumia muda mwingi wakati unaitumia kwani ni rahisi sana kuitumia. Kama haitoshi utaweza kutuma moja kwa moja picha hiyo kwenda katika mtandao wa Instagram

Shusha Hapa — Android

Kwa Wale Wa iOS.

  1. Instagrids

Instagrid Kwa iOS

Kama ni mtumiji mzuri wa iPhone (iOs) basi App hii ndio chaguo lako. Inakupatia urahisi wa kugawanya picha yako katika vipande pande ambavyo unaweza ukavipost na kuwa na muonekano tofauti katika profile lako. Kutuma kazi yako moja kwa moja katika mtandao wa Instagram inawezekana hivyo hautakuwa na haja ya kuhifadhi kazi zako katika gallery kwanza

SOMA PIA:  Udukuzi kwenye Instagram; Akaunti za watu maarufu zaingiliwa!

Hii inakuja katika matoleo mawili, Toleo la bure na lile la kulipia. Katika lile la kulipia unaweza ukapata huduma za kuongeza stika katika picha, unaweza ukaongeza rangi katika  vipande unavyotaka na mengine mengi. Kwa kifupi ni kwamba katika toleo la kulipia unaweza ukafanya uhariri (Edit) picha zako.

Shusha Hapa — iOS (Bure)

Shusha Hapa — iOS (Kulipia)

Mpaka hapo natumaini Profile lako linaweza likapata muaonekano wa kivyake. Kama umeshawahi kutumia App hizi au zinazofanana na hizi pia usisite kutuambia mapokezi yako.

SOMA PIA:  Facebook yaleta Messenger kwa ajili ya watoto chini ya umri wa miaka 13

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini sehemu ya comment —  hii unaionaje kama uko tayari kuitumia au la?

Kumbuka Kutembelea TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com