Facebook imejiboresha zaidi, safari hii inawawezesha watumiaji wake kuweza ku’post’ kwa kutumia lugha zaidi ya moja
Hapa unaweza jiuliza kwanini mtandao huo tishio (kwa mingine) umeamua kufanya hivyo. Dhumuni kubwa ni kuweza kuwaunganisha watu ambao wanatofautiana katika lugha.
Mara ya kwanza kabisa Facebook walianzisha kipengele hichi kwenye page maalumu (Fan Page) lakini kwa sasa wameamua kuwa kila mtu anaweza akatumia
Kwa kutumia kipengele hiki mtu anaweza andika ‘post/status’ moja kwa kizungu na kisha akaamua kuchagua lugha nyingine ambazo anataka ‘post/status’ hiyo isomeke. Watu ambao wanatumia lugha hizo ambazo umezichagua basi watakuwa na uwezo wa kuiona ‘post/status’ kwa kutumia lugha zao
Kujua Namna Ya Kupost Kwa Kutumia Lugha Tofauti Endelea Kusoma
>. Ingia katika ukurasa wako wa Facebook na kisha nenda moja kwa moja katika eneo la ‘Settings’
>. Katika upande wa kushoto ingia sehemu ya ‘language’. Katika upande wa kulia utaona ‘Multilingual Posts’ kama iko ‘Turned Of’ unaweza kuiwasha kwa kwenda katika ‘Edit’
>. Weka tiki kwenye kiboksi cha “Create a single post in multiple languages” na kisha chagua ‘Save’
>. Baada ya hapo jaribu kupost kitu chochote katika ukurasa wako utaona chaguo la kuandika post kwa kutumia lugha nyingine (Write a post in another language)
Mpaka hapo utakuwa ni mtaalamu wa kufanya jambo hili. Kumbuka hili ni jambo jema sana kutoka katika mtandao wa Facebook na haswa kama ukiwa na marafiki ambao wanatumia lugha nyingine tofauti na wewe