PowerShake: Teknolojia ya kushare chaji kwa kutumia Wi-Fi #Maujanja

0
Sambaza

Uwepo wa simu janja umekuwa na changamoto kadhaa hasa kwenye suala la simu janja kutokaa na chaji kwa muda mrefu na kutokana na changamoto ndio wazo la kushare chaji kwa Wi-Fi lilipozaliwa.

Njia za kuchaji simu janja zimezidi kuongezeka kila leo kwani siku hizi tunaweza kuchaji simu janja kwa kutumia “Power bank“, kwa kutumia umeme wa Jua ambazo zinakuwezesha kuchaji simu ingawa utumiaji wa vitu hivyo vinaongeza uzito katika ubebaji na vinahitaji umakini ili kuvilinda kutoharibiwa kwa sababu ni rahisi kuharibika. Watafiti wa mambo ya kiteknolojia wamekuja na teknolojia inaitwa “PowerShake“.

SOMA PIA:  Mwanasayansi agundua Viwavi jeshi wanaokula Plastiki na kuozesha ndani ya wiki

PowerShake ni nini?

PowerShake ni teknolojia inakuwezesha kushare chaji na mwenzako ili kuweza kuchaji simu ambayo imeishiwa na umeme. Ili kuweza kufanikisha ili simu zote mbili lazima ziwe simu janja, Wi-fi iwepo “On“.

Simu janja ikichajiwa kwa kutumia Wi-Fi

Simu janja ikichajiwa kwa kutumia Wi-Fi

Watafiti wanasema kuwa changamoto wa teknolojia hii ni kwamba nguvu inayotoka kwenye simu janja ni mara mbili zaidi kuliko na chaji inayoingia kwenye simu janja inayochajiwa. Ukichaji simu kwa muda wa sekunde 12 kwa kutumia teknolojia ya PowerShake inaweza unaweza kuongea kwa dakika moja ya ziada. Na kama ukichaji kwa muda wa dakika 2, unaongea kwa njia ya video kwa muda wa dakika nne.

Simu janja inayochajiwa Kwa kutumia Wi-fi ambayo ni shared

Simu janja inayochajiwa Kwa kutumia Wi-fi ambayo ni shared

Majaribio ya awali yanaonyesha kuwa teknolojia hii itasaidia sana kwani itakuwezeha kushare chaji na mtu na kuchaji sehemu yoyote na wakati wowote.

Je, unadhani teknolojia hii itadumaza soko la chaji za simu janja? Tuambie katika comment kwa kuandika maoni yako kuhusu suala hili. Hii ndio TeknoKona, daima tunakuhabarisha.

Vyanzo: psfk, Live science

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com