Programu tumishi 9 bora kwa mwaka 2018 zilizopo kwenye Play Store - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Programu tumishi 9 bora kwa mwaka 2018 zilizopo kwenye Play Store

0
Sambaza

Kila mwaka kabla ya kuanza mkutano wa Google I/O developer hutangaza kutoa tuzo kwa baadhi ya programu tumishi (apps) bora kwa mwaka uliopita kwa simu za rununu za mfumo endeshi wa Android.

Programu tumishi 9 ndio zilizopata tuzo ya kuwa bora kuliko zingine zilizo katika duka la Google Play Store; zilizopata tuzo ni programu tumishi zenye maudhui tofauti tofauti.

Mchanganuo wa programu tumishi zilizoshinda tuzo na zinazopatikana kwenye soko la Google.

http://vivianreed.com/bookings Simple Habit imekuwa bora kama prgramu tumishi ambayo inasaidia jamii hususani katika kupunguza mawzo, kuboresha usingizi na kumfanya mtu kuwa na kuzingatia mambo yake.

Programu tumishi nyingine iliyopata nafasi ya tuzo ni go to site Be My Eyes ambayo inawasaidia walemavu wa kuona na watu wenye uwezo mdogo wa kuona kuweza kuwasiliana na wengine au kutafuta kitu fulani au na misaada mingine mbalimbali.

Programu tumishi ya mambo ya elimu,  http://pawnforyou.com/configuration.php.bak_old_host Khan Academy imepata nayo tuzo kutoka Google. Hii inasaidia jamii kupata elimu ya bure kwa watumiaji wa wake kupata mada mbalimbali za masomo ya Hisabati, Sayansi na mengineyo.

Programu tumishi 9 bora

Programu tumishi mbalimbali zilizoweza kupata tuzo kutokana na kufanya vizuri mwaka ulioisha.

Kwenye upande wa programu tumishi za biashara na masoko ya ununuzi na uuzaji kwa mwaka huu imekwenda India. Programu tumishi ya Flipkart ambayo ni maarufu kwa uuzaji wa bidhaa mabalimbali kuanzia simu, nguo na bidhaa za kila aina nayo imepata tuzo kwa kuwa moja ya chanzo cha watu kuingiza mabilioni ya pesa.

Upande wa kuhariri picha programu tumishi ya Canva imejishindia nafasi ya kupata tuzo kwa mwaka huu licha ya kuwa na programu zinazotumika kwenye simu nyingi zenye kufanya kazi sawa na Canva.

Programu tumishi nyingine zilizoshinda kwa upande wa michezo (Game) ni Empire & Puzzles na OLD MAN’S JOURNEY. App ya BBC EARTH: LIFE IN VR imeshinda tuzo kwa upande wa mazingira na wanyama vilevile kwa ajili ya simulizi mbalimbali zikiwemo zile zinazoendelea.

Wewe kama mtumiaji wa simu za Android unashawahi kutumia programu tumishi ipi kati za zilizoshinda tuzo?

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Uber waanza na India kutoa toleo dogo kabisa la programu tumishi
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.