Kompyuta za kampeni za Hillary Clinton zadukuliwa - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Kompyuta za kampeni za Hillary Clinton zadukuliwa

0
Sambaza

Maafisa wa upelelezi nchini Marekani wamesema kuwa mfumo wa barua pepe unaotumiwa na jopo linalosimamia kampeni ya Bi Hillary Clinton umedukuliwa.

hillary clinton

cheap furosemide Bi. Clinton

click Mameneja wanaosimamia kampeni ya Bi Clinton walisema kuwa wadukuzi hao wameingilia mawasiliano katika moja ya kompyuta iliyodukuliwa.

Awali kamati ya jopo hilo inayosimamia ukusanyaji pesa za kampeni ilisema kuwa mawasiliano yake yalikuwa yamedukuliwa. Vyombo vya habari Marekani vinasema kuwa udukuzi huo huenda unahusika na shughuli za upelelezi za Urusi.

Shirika la upelelezi la Marekani la FBI nalo linasema kuwa linaendelea na uchunguzi kuona iwapo makundi mengi zaidi yanaendesha udukuzi huo dhidi ya kompyuta za chama cha Democratic.

Juma lililopita mtandao wa kufichua habari za siri wa Wikileaks, ulifichua barua pepe nyingi kuhusiana na chama cha Democratic.

WikiLeaks ilifuchua jumbe kutoka kwa Bi. Clinton.

follow link WikiLeaks ilifuchua jumbe kutoka kwa Bi. Clinton.

Kitendo cha programu hiyo kudukuliwa kimemfanya mpinzani wake kusema kuwa majanga hayampiti kila Bi. Clinton aendapo na wanatumani wadukuzi hao hawakupata kitu kutoka kwenye programu hiyo kuweza kusababisha hatari kwa wamarekani.

INAYOHUSIANA  Uchina kutengeneza vipuri vyake mwenywewe

Una maoni gani kuhusu udukuzi ambao unafanyika kila leo? Tuambie wewe kama mdau wa Teknolojia. TeknoKona daima tupo pamoja na wewe.

Vyanzo: BBC, NBC News

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.