Q Control: Toleo jipya la saa janja kutoka Fossil

0
Sambaza

Fossil imekuwa ni moja ya makampuni ambayo yanashindana vilivyo na kampuni kama Apple kwenye biashara ya saa janja na baada ya kutoa toleo lililopita katika muendelezo wa saa janja kutoka kwenye familia ya “Q”.

Fossil wamekuwa wakijitahidi kuleta utofauti wa toleo moja hadi jingine na kwa upande wa saa janja Q Control ina vile vitu ambavyo havikutokea kupendwa katika toleo lililopita la saa janja na hata kuthubutu kuongezea kitu kipya ambacho hakikuwahi kuwepo kwenye saa janja zote kutoka Fossil.

Yaliyomo kwenye saa janja ya Fossil (Q Control).

Muonekano. Q Control muonekano wake ni wa kuvutia ikiwa imewekewa kitufe kimoja tu; ina kioo cha mguso ambacho ni kipana kwa kumuwezesha mtumiaji aweze kuperuzi kwa urahisi bila kuona kioo ni kidogo na kuwa changamoto kidogo kuweza kuitumia saa janja kutoka Fossil.

Wembamba wake ni 13.5mm na ukubwa wa kioo ni 14.5mm ambacho kina mguso wa aina yake pembezoni mwa saa yenyewe ambao ni mahusu kwa kumuwezesha yule aliyeivaa saa hiyo kuweza kuperuzi programu tumishi mbalimbali. Unaweza kubadilisha mikanda yake kwa urahisi kabisa; ukiinunua inakuja na jozi moja ya ziada ya mikanda.

Q Control: Muonekano wa saa janja kutoka Fossil.

Programu endeshaji. Toleo jipya la saa janja kutoka Fossil inatumia Android Wear 2.0 yenye uwezo wa kuunganishwa na simu janja yoyote inayotumia kuanzia Android 4.4 au iOS 9 na kuendelea. Ina prosesa ya Qualcomm Snapdragon Wear 2100 na RAM GB 4.

SOMA PIA:  Apple Kuja Na Emoji Mpya Katika Vifaa Vya iOs na macOS!

Bei na sifa nyinginezo. Saa hii ni nzuri na inavutia na kulingana na uwezo wake inauzwa kwa $275|Tsh. 618,750 (kwa bei ya ughaibuni). Ina Bluetooth na uwezo wa kupata Wi-Fi. Ukishaiunganisha na simu janja una uwezo wa kupokea na kujibu ujumbe mfupi wa maneno kupitia Q Control. Tazama picha jongefu kujua mengi zaidi kuhusu saa janja kutoka Fossil. 

Q Control ndio saa janja ya kwanza kutoka Fossil kuwa na uwezo wa kupima mapigo ya moyo kama zilivyo saa janja nyingine kutoka makampuni mbalimbali. Je, umevutiwa na saa hii? Tayari imeshaanza kuuzwa ila ni kwa kuagiza kupitia masoko mbalimbali ya mtandaoni.

Vyanzo: Trusted Reviews, Techradar, Android Police

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com