QIK: App Mpya Ya Video Kutoka Skype!

0
Sambaza

microsoft-launches-skype-qik-video-chat-app-for-android-ios-windows-phone

Wewe ni Mpenzi wa Skype? Mimi napenda sana app hiyo. Skype ni programu inayomilikiwa na Microsoft, ile kampuni inayomilikiwa na Bill Gates. Kama Skype jinsi ilivyo, Qik inakuwezesha kutuma video tuu kwa familia, marafiki zako na namba nyingine kwenye simu yako. Ukishamaliza ku’download’ hii aplikesheni (Kwenye iOs, Android na Windows Phone), unajisajili na namba yako ya simu na utakuwa mzigoni. Unaweza kutumiana meseji mmoja kwa mmoja au kwenye kundi. Unataka nini tena? Hii ndio digital uliyokua unaiulizia kipindi cha nyuma sio?

“Watumiaji wengi wa skype wanaitumia kwenye simu zao za mkononi na sio kwenye kompyuta zao hata wale watumiaji wapya” alisema Mtendaji wa Skypa Bw. Dan Chastney

App hii ni rahisi kufunguka, ku-load na kuitumia. Kuna kibonyezo kimoja tuu cha kurekodi meseji yako. Gusa mara ya kwanza kwa kuanza kurekodi ujumbe wako, gusa mara ya pili kustopisha na kutuma. Kama hujapenda jinsi ulivyorekodi hiyo video fupi unaweza ukafuta na kuanza tena. Unaweza kutumia kamera ya nyuma na ya mbele kwenye simu yako kama ilivyo kwenye Skype.

SOMA PIA:  Zanzibar kuzima mitambo ya Analogia kwenda Digitali Agosti 31, 2017

iphone-receiving

Unaweza kutuma meseji kwa mtu yeyote kwenye simu yako na kama hana hii app, atapata meseji inayomuomba aishushe app hii kwenye soko la app ya simu yake. Meseji zinahifadhiwa kwa wiki mbili tuu na baada ya hapo zinajifuta zenyewe. Bw. Chasteny amasema kuwa, app hii imetengenezwa ili kufanana na Skype lakini lakini ikiwa na utofauti wa pekee. App hii ina logo kama ya Skype ijapokua yenyewe ina rangi ya pinki wakati Skype ina rangi ya bluu. Pia amesema app hii haitakua ya kumaliza chaji kwenye simu yako kwa haraka.

SOMA PIA:  Binti afariki akifanyiwa upasuaji kuongeza makalio!😯😯😯

 

Meseji yoyote unayotuma unaweza kufuta katika kifaa chako (simu au tableti) na pia kwa kila mtu katika uwanja wa meseji. Meseji zitabaki pale pale kwenye uwanja wa mazungumzo, huwezi kuzisave, kuzifowadi na hata kuzi posti facebook (ha!). Wamefanya hivyo ili kusaidia watumiaji wa app hii kuwa na uwezo na nguvu juu ya vitu wanavyoongelea baina yao. Hakuna mtu anaependa kuongea siri na mwenzie ili baadae aikute ipo wazi katika mitandao ya kijamii.

SOMA PIA:  Q Control: Toleo jipya la saa janja kutoka Fossil

Skype-Qik-app-windows-phone-header-2

 

Hii app Imeachiwa hewani Tarehe 14 Mwezi Oktoba, 2014. Lakini Qik ilikua ni app ya kujitegemea miaka ya nyuma na ni kabla ya kununuliwa na Skype Januari 6, 2011 kwa dola za kimarekana milioni 150

 

Kingine Kipya Kutoka Microsoft! Tafadhali Toa Comment Yako Hapo Chini, Tuambie Umekipokeaje?

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com