Rais JPM atamba kutumia mitandao yote ya simu

0
Sambaza

Rais John Magufuli amesema anajivunia kuwa na mitandao mingi ya simu ambayo inamsaidia kuwasiliana bila kero wakati wowote.

Amesema hayo leo Jana, wakati wa uzinduzi wa mfumo wa ulipaji kodi kwa njia ya kielektroniki.“Mimi nina mitandao yote ya simu, nina Tigo, Airtel, Vodacom na hata TTCL, mtu akinitafuta huku Airtel, akanikosa ninaweza kuweka Tigo, ili mradi ninatambulika kila mahali,” amesema.

Rais JPMagufuli

Rais John Magufuli

Pia amesema, mitandao hiyo ya simu inamsaidia kupata taarifa mbalimbali zinazoendelea nchini na duniani.Hata hivyo, Rais amezitaka kampuni za simu kuhakikisha zinalipa kodi ili serikali isikose mapato yake.

Pia Rais amesema hataki kuona taasisi nyingine zinajenga vituo vya ukusanyaji taarifa (Data centre)na badala yake  fedha hizo zitumike kwa ajili ya shughuli nyingine za maendeleo.

“Data Centre kama hii ni mkombozi mwingine wa kupunguza kero mbalimbali, kwa sababu ukijaza vocha yako uko Zanzibar, ukinunulia vocha yako Kigoma au Moshi, hiyo pesa inakuja TRA, hakuna mabishano” amesema.

Rais amesema hayo, wakati wa uzinduzi wa mfumowa wa serikali wa ulipaji kodi kwa njia ya kielektroniki ambako pia alitembelea kituo hicho cha ukusanyaji taarifa.

SOMA PIA:  Google na Microsoft waungana katika vita dhidi ya mitandao ya mafaili ya wizi

Amesema chombo hicho kina faida yake na hivyo akawaomba watanzania, wawekezaji na wafanyabiashara kukitumia chombo hicho kwa manufaa ya taifa zima.

Chanzo: Mtanzania

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com