Rais wa kampuni ya simu za HTC ajiuzulu - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Rais wa kampuni ya simu za HTC ajiuzulu

0
Sambaza

Baada ya kampuni ya Google kuwanunua wahandisi wake takribani 2,000 na kupata fedha nyingi, sasa kampuni ya utengezaji wa simu janja za HTC imepata pigo jingine kwa aliyekuwa rais wa kampuni hiyo kuachia ngazi nafasi hiyo ya urais.

purchase augmentin online

http://grangevillegolf.com/idaho-golf-clubs/news/?print=pdf-search Bw. Chialin Chang alijiunga na HTC tangu mwaka 2012 ametangaza kujiuzulu nafasi ya mwenyekiti na mkurugenzi Mtendaji na kuamua kufanya shughuli zake za kibinafsi.

http://castlerockelectricalcontractor.com/how-to-choose-an-electrical-contractor/ Bw. Chialin Chang aliyekuwa rais wa HTC akiwa katika uzinduzi wa simu rununu HTC U11+.

Mpaka sasa HTC haijatangaza ni nani atachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Chialin Chang.

Aidha, HTC imetoa taarifa ya kuthibitisha kujiuzulu kwa Bw. Chialin Chang kutoka nafasi ya Urais kwa kumshukuru kujitolea kwake kwa kampuni hiyo kwa muda wa miaka sita na kumtakia mafanikio katika shughuli zake mpya.

Kujiuzulu kwa Chialin chang sio jambo la kushangaza licha cha kuja katika kipindi kisichofaa. HTC imekuwa ikipoteza thamani yake katika miaka ya hivi karibuni.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.