Raisi wa waTanzania walio Twitter (TOT) apatikana - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Raisi wa waTanzania walio Twitter (TOT) apatikana

0
Sambaza

Hatimaye mzee mzima Rickyboshe (@Rickyboshe) aka comic boy ametangazwa mshindi wa kinyang’anyiro cha kumsaka raisi wa waTZ walio katika mtandao wa twitter ama kwa kimombo Tanzanians On Twitter(TOT).

can you buy finast in uk

TOT

follow link Picha ya umbo ya akaunti ya Raisi mteule wa TOT. @rickyboshe twitter

@Rickyboshe ambaye alijikusanyia kura 352 amewakimbiza wapinzani wake wawili Mussa barry (@somebarry) aliepata kura 319 pamoja na msupuu Daisy (@omalichaa_) ambaye alipata kura 105.

Kama katika chaguzi nyingine nyingi kuna kundi la watu bado wanaona mgombea wao mmoja alistahili zaidi ushindi…

Kama bado ulikuwa hujui TOT ni moja kati ya makundi ambayo yananguvu kubwa ya ushawishi katika mitandao ya kijamii, tayari kikundi hiki kimekwisha fanya mambo mengi ambayo yamekuwa na mchango wa moja kwa moja katika jamii mfano uchangiaji katika harambee tofauti tofauti zinazogusa jamii ama mtu mmoja mmoja. Ingawa wapo ambao wanaamini hiki ni kikundi cha watu wachache kwa manufaa yao lakini ukweli ni kwamba kama wewe ni mTanzania na upo Twitter basi u mmoja wa wanaTOT.

TOT

Picha ya umbo ya akaunti ya @somebarry akiwa anajipigia kampeni.

Uchaguzi huu uliigawa TOT katika makundi matatu kulingana na wagombea wa nafasi hiyo ya uraisi walivyokuwa, @somebarry yeye alikuwa akifananishwa na aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Uraisi wa Tanzania mwaka jana bwana Lowassa alikuwa kipata  uungwaji mkono mkubwa na wana TOT ambao walikuwa wanaamini kwamba ni wakati mabadiliko yafanyike katika namna nzima watumiaji wa mtandao huu wanaweza kushirikiana na kufanya mambo mbali mbali.

INAYOHUSIANA  Waliopewa dhamana ya kusimamia mifumo ya TEHAMA serikalini waonywa na kutakiwa kuzingatia weledi kazini

@omalichaa_ alipata uungwaji mkono saana na wa-Beijing wengi na kauli mbiu yake ilikuwa ni haki sawa kwa wote, kwake mshindi ambaye sasa ndiye raisi mteuliwa @rickyboshe yeye alipata uungwaji mkono kwa watu ambao hawakuwa wafuasi wa makundi mawili yaani sio Side Z wala sio mwana woke twitter.

TOT

Picha ya Umbo ya @omalichaa_ wakati wa kampeni

Aidha @somebarry ameibuka baada ya matokeo kutangazwa na kusema kwamba kura 63 zimeharibika baada ya watu kukiuka masharti ambapo waliandika Mussa badala ya kuandika @somebarry yaani walitumia jina badala ya handle kitu ambacho kamati ya uchaguzi imesisitiza kwamba kura iki haribika haiwi ya mgombea mmoja bali wote wanakuwa wameipoteza. kwa upande wake mgombea pekee wa kike @omalichaa_ yeye amekubali matokeo na kumpongeza mshindi.

INAYOHUSIANA  Halopesa-Halopesa ni bure! Halotel-Mitandao mingine inavutia

enter Makampuni ya simu na mengine mbalimbali hayakuwa nyuma kujihusisha na uchaguzi huo

Teknokona inasimama pamoja na wana TOT wote kumpongeza mshindi raisi mteule @rickyboshe na katika umoja huo tunawapongeza wote walioshiriki katika uchaguzi huu kwa nafasi ya pekee @omalichaa_ na @somebarry, TOT ni moja makundi yaishie katika utani na parody.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

Comments are closed.