Hivi ni mara ngapi ulisharekodi video zile za Instagram/Snapchat lakini vidole vikakuharibia (mfano, ukaifuta kwa bahati mbaya)? Licha ya hivyo tuu kuna muda mwigine tunashindwa kushika simu zetu vizuri na kupata ‘angle’ nzuri ya kurekodi video hizo.
Sasa kama wewe ni mtumiaji wa iPhone utakuwa na uwezo wa kufanya video hizo zijirekodi zenyewe wakati wewe ukiwa umetegesha simu tuu. Baada ya hapo utaweza kuzituma picha/video hizo katika mitandao yako ya kijamii (Instagram/Snapchat).
Fuata Haya.
1. Fungua sehemu ya Settings na kisha chagua General na kisha Accessibility.
2. Chagua Assistive Touch kwenye sehemu ya Interaction na kisha iwashe.
3. Bonyeza na kisha chezesha kidole (huku umeshikilia kioo) ili kutengeneza umbo la duara.
4. Baada ya hapo unaweza uka’save’ na ukaandika jina (video) lolote unalotaka.
5. Baada ya hapo utakuwa umeshaweza hatua ya kwanza. Sasa kilichobakia ni wewe kwenda katika mtandao wa Instagram/Snapchat.
– Ukishafunguka uwanja wa kupiga picha/video, bonyeza kile kiduara cha Assistive Touch alafu nenda katika Custom na kisha Video (au jina lolote ulilolihifadhi mwanzo)
6. Baada ya hapo utakiona kiduara kingine kidogo kimejotokeza, hapo unatakiwa kukishikilia na kukisogeza katika duara kubwa la kupigia picha la Instagram/Snapchat na kisha utashuhudia maajabu ya teknolojia.
Mpaka hapo na wewe umeshakuwa mtaalamu sio? Kumbuka utakuwa huna haja tena ya kuanza kubonyeza kile kiduara katika Snapchat/Instagram Ili kuredi video. Hapa utakuwa kama bosi hivi, utashika tuu simu huku yenyewe ikifanya yake.