Rekodi mpya ya kasi ya intaneti ya mfumo wa 4G imewekwa.
Kampuni ya Finland Elisa inasema imefanikiwa kupata kasi ya Gigabait 1.9 kwa sekunde, ikisema hiyo ndio kasi ya juu zaidi kuwahi kupatikana. Mwezi Februari jopo la wanafunzi waliokuwa wakifanya utafiti waliweza kugundua kizazi cha 5 katika intaneti (5G) yenye kasi ya 1Tbps ambapo kasi yake ni mara 50 bora zaidi ya 4G ingawa utafiti huo haukuwa rasmi.
Huduma hiyo ya intaneti yenye kasi zaidi inaweza kupakua Filamu ya Blu Ray kwa muda wa sekunde 44.
Lakini wachanganuzi wana wasiwasi kwamba kasi hiyo inaweza kutumika moja kwa moja katika mtandao halisi ulimwenguni.
Elisa imesema kuwa imetumia teknolojia iliotolewa na kampuni ya China ya Huawei kutoa kasi ya upakuzi katika mtandao wa simu uliokaribia kiwango cha 2Gbps. Elisa wana mipango ya kuanzisha intaneti yenye kasi ya 1Gbps nchini Finland miaka 3 ijayo.
Ukilinganisha kasi ya 3G mtandao ni 300Mbps ambayo iko chini mara sita na mpaka sasa hakuna kasi kama hii iliotangazwa na mitandao mingine.
Je, makampuni yetu ambayo yanatoa huduma ya intaneti yanakaribia kufika kasi ya 1.9Gbps? Kama hakuna mategemeo ya kufika hapo basi hili iwe chachu kwa makampuni yote yaliyopo ndani na nje ya Tanzania.
Vyanzo: BBC, International Business Times
One Comment
Comments are closed.