Kwa mujibu wa ripoti iliyozinduliwa na Google idadi ya wakenya wanaonunua na kuuza bidhaa kupitia mtandao wa intaneti imeongezeka kwa asilimia 14 tangu 2014.
Utafiti huo uliofanywa na Kantar TNS, ripoti hiyo Consumer Connected Study 2017 inaonyesha kuwa ongezeko hilo ni kubwa sana.
Hii ni kutokana na kuwa mwaka wa 2014 idadi ya wananchi waliokuwa wakinunua bidhaa ilikuwa ni asilimia tatu pekee. Kufikia sasa, asilimia 53 ya wananchi walio na umri wa miaka 16 na zaidi wanaweza kutumia intaneti.
Asilimia hiyo imeongezeka kutoka asilimia 49 mwaka wa 2016. Kenya ni taifa la tatu lililo na watumiaji wengi zaidi wa intaneti ikilinganishwa na Afrika Kusini (asilimia 65) na Nigeria (asilimia 63).
Kwa mujibu wa afisa wa uhusiano mwema wa Google Africa Bi. Dorothy Ooko licha ya kuimarika katika matumizi ya intaneti, wananchi wengi hawana uzoefu.