RIPOTI: Huawei Wanatengeneza OS Yao Wenyewe Kama Tahadhari! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

RIPOTI: Huawei Wanatengeneza OS Yao Wenyewe Kama Tahadhari!

0
Sambaza

Ripoti zilizopo ni kwamba kampuni ya Huawei inatengeneza Programu-endeshaji yake yenyewe kama vile tahadhari kama mambo yakienda kombo baina yao na Google ambao wanamiliki program-endeshaji ya Android.

buy inderal in australia
Mpaka sasa Huawei ni kampuni Kubwa la tatu kwa utengenezaji wa simu janja duniani kote. Simu za Android zinatumia programu-endeshaji ya Android.

Huawei

here Huawei

http://growingwell.org/our-stories/page/2/ Ni sawa kabisa kuwa simu janja nyingi siku hizi zinatumia Android lakini hili bado haliwaogopeshi Huawei. Pia kumbuka kuna makampuni kama vile Apple ambao wanatengeneza simu janja za iPhone wana OS ya kujitegemea wao kama wao na wanafanya vizuri sana katika soko la simu na kompyuta kwa ujumla

INAYOHUSIANA  Huawei waendelea kutoa toleo jingine la simu za Honor

Ripoti imetoka ikisema kuwa timu kutoka Huawei inatengeneza Os ya simu huko nchini Sweden kwa kushirikiana na wafanyakazi wa zamani wa kampuni ya Nokia

Jambo hili inabidi lisikushangaze kabisa hivi ushawahi kufikiria kama makampuni haya mawali (Huawei na Google) yakigombana nini kitatokea? Inamaana mamilioni ya simu kutoka Huawei yatakuwa hayatumiki? Kumbuka Google ndio Android!

Hvi ni vizuri kwa kampuni yeyote kuwa na plani nyingine kama jambo kama hili litatokea haswa kwa kampuni kubwa kama Huawei

Kampuni kwa sasa ni moja kati ya makampuni kubwa sana duniani katika soko la simu janja. Moja kati ya lengo lake kubwa kwa sasa ni kuweza kuweka saini na kampuni lolote kubwa la mtandao huko marekani kama vile AT&T, Verizon, T- Mobile au Sprint

Baadhi Ya Simu Za Huawei

Baadhi Ya Simu Za Huawei

Pia kumbuka katika masoko ambayo yameendelea huwa watoi sifa kubwa kwa makampuni ambayo yametoa bidhaa ambayo bado kwa namna moja au nyingine bado inatumia kipengele kingine kutoka kampuni nyingine katika bidhaa hiyo (Yaani Huawei Inatumia Android)

INAYOHUSIANA  VLC haipatikani kwa baadhi ya simu za Huawei

Kama simu hiyo ingekuwa inajitegemea kwa kila kitu mpaka Os basi katika ingepata sifa kedekede katika masoko ambayo yameendelea.

Kwa mfano wakati simu za BlackBerry na Nokia zilisifiwa sana wakati zilipokuwa zinatumia OS zake zenyewe. Watu wengi waliposikia Blackberry wanarudi na OS ya Android walikohoa kwanza kabla ya kukubaliana na matokeao.

Kwa mtazamo wangu naona kabisa kuwa kampuni la Huawei linafanya maamuzi sahihi. Ningependa kusikia kutoka kwako nini maono yako juu ya swala hili? Niandikie hapo chini sehemu ya comment.

Tembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona kila siku kwa habari na maujanja mbalimbali yanayohusu Teknolojia kwa ujumla. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.